Ten Hag anarudi Ajax

Muktasari:

  • Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag amefunguka yupo tayari kurudi tena Uholanzi na kuifundisha Ajax endapo ataondoka kwa mashetani hao wekundu.

MANCHESTER, ENGLAND: Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag amefunguka yupo tayari kurudi tena Uholanzi na kuifundisha Ajax endapo ataondoka kwa mashetani hao wekundu.

Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag amefunguka yupo tayari kurudi tena Uholanzi na kuifundisha Ajax endapo ataondoka kwa mashetani hao wekundu.

Ikiwa msimu utamalizika vibaya kwa Man United na wakapoteza mechi fainali ya FA dhidi ya Manchester City inaweza ikasababisha Ten Hag kufungashiwa virago na kufukuzwa.

Mara kadhaa amekuwa akihusishwa na timu yake ya zamani Ajax ambayo kwa sasa inatafuta kocha baada ya kumfukuza Maurice Steijn Oktoba mwaka jana kisha akapandishwa John van’t Schip kukaimu nafasi hiyo lakini kiwango cha timu chini yake hakijaonekana kuwavutia mabosi wa Ajax na kuendelea kumbakisha. stepping down.

Akizungumza na  ViaPlay, Ten Hag alisema: “Hakuna mazingumzo yoyote niliyofanya na Ajax kwa sasa lakini hapo baadae inawezekana, ni timu nzuri na nilikuwa na nyakati nzuri sana pale”

Hata hivyo, Ten Hag haoni kama anaweza kurudi kwenye timu hiyo kwa msimu ujao kwani anaamini ataendelea kuwepo Man United.

“Nafikiri nitakuwa kocha wa Manchester United kwa mwaka ujao, nilisaini mkataba wa muda mrefu tena kwa umakini, mimi sio mtu ninayeweza kukimbia tu.”

Hadi sasa mkataba wa Ten Hag umebakisha mwaka mmoja na inaelezwa inawezekana usiishe akawa tayari ameshaondolewa.

Mara kadhaa kocha wa zamani wa Chelsea,  Graham Potter na kocha wa England Gareth Southgate wamewahi kutajwa kwamba wapo kwenye mipango ya kuajiriwa kuchukua nafasi yake.