Tarehe ya Kombe la Dunia yabadilishwa

Muktasari:

  • SHIRIKISHO la mpira wa miguu Duniani (FIFA), limerudisha nyuma tarehe ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu itakayofanyika nchini Qatar, ili kuipa nchi mwenyeji kucheza mechi ya ufunguzi.

DOHA, QATAR. SHIRIKISHO la mpira wa miguu Duniani (FIFA), limerudisha nyuma tarehe ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu itakayofanyika nchini Qatar, ili kuipa nchi mwenyeji kucheza mechi ya ufunguzi.
Awali tarehe ya kuanza kwa michuano hii ilikuwa ni Novemba 21, ambapo mchezo wa kwanza ungekuwa kati ya Senegal na Uholanzi.
Lakini Qatari ilituma maombi ya mchezo wao wa Novemba 21, dhidi ya Ecuador uchezwe Novemba 20 ambapo utakuwa mchezo huo pekee na kuwaruhusu kufanya sherehe za ufunguzi.
Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Mail , ratiba mpya inaonyesha kwamba Qatar itacheza na Ecuador saa 1:00 usiku kwa saa za afrika ya mashariki katika uwanja wa  Al Bayt Stadium.
Mchezo pekee ambao umerudishwa nyuma ni huo wa mwenyeji Qatar, hivyo mechi nyingine zote zitaendelea kama ilivyokuwa hapo awali.