Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stones nusura astaafu soka

Muktasari:

  • Stones, 31, alishuhudia msimu wa 2024-25 akiwa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya mguu na misuli ya paja. Aliicheza mechi 24 kwa klabu yake na nchi yake na hakucheza mechi yoyote tangu Februari.

MANCHESTER,  ENGLAND: BEKI wa kati wa Manchester City na England, John Stones amefichua alifikiria kustaafu soka msimu uliopita baada ya kuandamwa sana na majeraha.

Stones, 31, alishuhudia msimu wa 2024-25 akiwa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya mguu na misuli ya paja. Aliicheza mechi 24 kwa klabu yake na nchi yake na hakucheza mechi yoyote tangu Februari.

Lakini, sasa yupo fiti msimu huu na anajiandaa kuitumikia England katika mechi zijazo za kimataifa wakati England itakapokabiliana na Wales na Latvia.

“Msimu uliopita ulikuwa mgumu sana kwangu, ilifika kipindi nilifikiria kabisa kuacha,” alisema Stones. 

Licha ya kusumbuliwa na maumivu msimu uliopita, Stones aliungana na kikosi cha Thomas Tuchel kwenye kipindi cha majira ya kiangazi alipoumia Andorra na Senegal.

“Naipenda sana England na ningependa kuichezea,” alisema Stones.

Beki huyo amekuwa na mafanikio makubwa kwenye kikosi cha Man City, ambapo kocha Pep Guadiola kuna nyakati nyingine amekuwa akitumika kwenye sehemu ya kiungo mkabaji.