Staa wa mchangani kuitwa kikosi cha Uruguay

Muktasari:

  • Kocha huyo wa zamani wa Leeds United amechukua mikoba ya kuinoa timu hiyo ya taifa ya Amerika Kusini tangu mwaka jana. Sasa yupo kwenye maandalizi ya kufuma kikosi chake kwa ajili ya mikikimikiki ya Copa America itakayofanyika kwenye kipindi cha majira ya kiangazi mwaka huu.

MONTEVIDEO, URUGUAY: Kosha wa mpira, Marcelo Bielsa amepanga kumjumuisha mchezaji wa mchangaji kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uruguay.

Kocha huyo wa zamani wa Leeds United amechukua mikoba ya kuinoa timu hiyo ya taifa ya Amerika Kusini tangu mwaka jana. Sasa yupo kwenye maandalizi ya kufuma kikosi chake kwa ajili ya mikikimikiki ya Copa America itakayofanyika kwenye kipindi cha majira ya kiangazi mwaka huu.

Lakini, katika mpango huo, timu hiyo inajiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Costa Rica, Mei 31.

Kinachoripotiwa ni Bielsa amempanga kumpa mchezaji wa mchangani, Walter Dominguez nafasi ya kucheza timu yake ya taifa. Straika huyo mwenye umri wa  miaka 24, anachezea Juventud de Soriano.

Hakika amekuwa kwenye kiwango bora katika timu yake hiyo, akifunga mabao 38 katika mechi 19.

Dominguez akiitwa atakwenda kucheza sambamba na staa wa Liverpool, Darwin Nunez na wa Real Madrid, kiraka Federico Valverde.

Bielsa amepanga kumpa nafasi mchezaji huyo baada ya kushindwa kuwaita mastaa wa timu za Nacional, Penarol, Racing na Danubia kwa sababu zipo kwenye mchuano wa ubingwa wa Copa Libertadores na Sudamericana.

Straika, Dominguez alisema: “Wamenipigia simu na nimefurahi sana. Sikutarajia kabisa na hii ni sapraizi.”