Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spurs yamchukua Tudor aokoe jahazi

Muktasari:

  • Inaelezwa kocha huyo wa Croatia amekubali mkataba wa awali hadi mwezi Juni na klabu hiyo ya Kaskazini mwa London.

LONDON,  ENGLAND: TOTTENHAM Hotspur imemgeukia Igor Tudor kuwa kocha wa muda hadi mwisho wa msimu.

Inaelezwa kocha huyo wa Croatia amekubali mkataba wa awali hadi mwezi Juni na klabu hiyo ya Kaskazini mwa London.

Hatua hiyo inafuatia kutimuliwa kwa Thomas Frank, Jumatano asubuhi, saa chache baada ya kipigo cha mabao 2-1 nyumbani dhidi ya Newcastle United kuiacha Spurs ikiwa pointi tano tu juu ya eneo la kushuka daraja.

Tudor, mwenye umri wa miaka 47, amefundisha klabu tisa tofauti katika nchi tano tangu alipoanza kazi yake ya ukocha na HNK Hajduk Split mwaka 2013. Hii itakuwa mara yake ya kwanza kufundisha nchini England kwa kocha huyo wa zamani wa Juventus FC.

Spurs ilitaka kocha wa muda mwenye uzoefu wa kuleta mabadiliko ya haraka katika klabu ili kuwasaidia kujinasua na hatari ya kushuka daraja.

Kisha itatafuta kocha wa kudumu wakati wa majira ya joto, ambapo kundi pana la wagombea litapatikana. Miongoni mwao ni kocha wao wa zamani anayependwa sana, Mauricio Pochettino, ambaye hawezi kujiunga hadi baada ya Kombe la Dunia 2026 atakapomaliza majukumu yake kama kocha wa timu ya taifa ya Marekani.

Lakini, kama Tudor ataonyesha mafanikio  kati ya sasa na mwisho wa msimu, atazingatiwa kwa nafasi hiyo kwa kudumu.

Tudor amewahi kufundisha klabu kama Galatasaray SK, SS Lazio na PAOK FC, huku kazi yake ya mwisho ikiwa Juventus ambao Spurs wanaweza kukutana nao katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Alikuwa kocha wa Olympique de Marseille wakati Spurs ilipowafunga mara mbili katika Ligi ya Mabingwa msimu wa 2022-23.

Pia alimfundisha mshambuliaji wa Spurs, Randal Kolo Muani wakati wa mkopo Juventus msimu uliopita. Tudor alichukua mikoba Turin wakati timu yake mpya ikiwa imepoteza mechi mbili za mwisho. Juventus iliendelea kupoteza mechi moja kati ya tisa Serie A na kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa. Hata hivyo, Tudor alitimuliwa na klabu hiyo ya Italia Oktoba mwaka jana baada ya miezi saba.