Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Solskjaer amfananisha Cavani na gwiji wa Man United

Kinachomuweka benchi Cavani hiki hapa

MANCHESTER, ENGLAND. KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amekoshwa na mavitu ya straika wake Edinson Cavani na kusema uzoefu na majukumu anayofanya kwenye timu yanafanana na ya gwiji wa zamani wa timu hiyo, Teddy Sherringham.

Sherringham raia wa England, alijiunga na Man United mwaka 1997, akitokea Tottenham alikochukuwa kiatu cha ufungaji bora wa Ligi Kuu England msimu wa 1992-93 na kujitambulisha kama straika hatari duniani.

“Teddy alikuja 1997 na uzoefu ambao nilijifunza kwake. Nadhani naye Cavani amekuja na aina ya ushawishi unao fanania,

Tulikuwa mastraika wachanga tuliojifunza kutoka kwa Teddy. Kwa sasa Cavani yupo na Mason Greenwood, Marcus Rashford, na Anthony Martial wanaojifunza kutoka kwake. Edinson amekuwa na mchango mkubwa,"alisema Solskjaer.

Solskjaer na Sherringham walifunga magoli mawili ya dakika za mwisho katika mechi ya kusisimua ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 1999 dhidi ya Bayern Munich. Man United ikiwa chini ya kocha Sir Alex Ferguson ilishinda mataji matatu mwaka huo.

“Amekuwa ni mfano, anafanya kazi yake kwa weledi, ni shauku yake, anapenda mpira wa miguu, anapenda kujituma kwa ajili ya timu. Kama akifanya makosa mara nyingi hujaribu kulifanyia kazi,” aliongeza Ole.

Akiwa Man United, Sherringham alishinda matatu ya Ligi Kuu England msimu wa 1998-99, 1999-2000 na 2000-01. FA  msimu wa 1998-99,  Ngao ya Hisani moja 1997, Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 1998-99 na Kombe la Mabara kwa ngazi ya klabu mwaka 1999. Aliondoka Man United mwaka 2001 na kurejea timu  Tottenham.

Cavani, 33, ambaye ni raia wa Uruguay, alijiunga na Man United Oktoba 5, 2020 akitokea PSG alikocheza kwa kiwango kikubwa na kuacha rekodi  yakuwa mfungaji bora wa muda wote.