Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot, Mo Salah kumaliza ishu yao kwa mazungumzo

SLOT Pict

Muktasari:

  • Mo Salah amekuwa akihusishwa na klabu za Saudi Arabia, ikidaiwa anaweza kunaswa kwenye dirisha lijalo la majira ya baridi ili kuondoka kwenye klabu ambayo imekuwa chungu kwake baada ya kutibuana na kocha Mdachi, Slot.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot amefichua kwamba atafanya kikao cha ana kwa ana na Mohamed Salah ili kufahamu msimamo wa mwisho kama atacheza mechi ya mwisho kwenye kikosi hicho cha Anfield.

Salah, 33, alidai kwamba mechi ya Jumamosi dhidi ya Brighton inaweza kuwa ya mwisho kwenye klabu hiyo baada ya kuzungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari na kuibua sintofahamu kubwa huko Anfield.

Staa huyo wa kimataifa wa Misri alidaiwa kumwalika mama yake uwanjani Anfield kuja kumshuhudia kwa sababu hiyo inaweza kuwa mechi yake ya mwisho kabla ya kuondoka kwenye timu hiyo.

Wiki ijayo, Salah atakwenda kuungana na Misri kwa ajili ya mashindano ya Afcon na michuano hiyo itakwisha mwezi ujao, kipindi ambacho dirisha la usajili la majira ya baridi litakuwa limefunguliwa.

Mo Salah amekuwa wakiwekwa benchi na kocha Slot kwenye kikosi cha Liverpool kwa mechi za hivi karibuni ikiwamo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Inter Milan, ambapo Liverpool ilishinda 1-0 uwanjani San Siro.

Na sasa katika kuuendea mchezo wa Brighton, Mo Salah aliripotiwa atakuwa na mazungumzo na kocha Slot huko AXA Training Complex, Kirkby ili kutambua nini kitafuata baada ya mechi hiyo na kile kilichozungumzwa na mchezaji huyo.

Mo Salah amekuwa akihusishwa na klabu za Saudi Arabia, ikidaiwa anaweza kunaswa kwenye dirisha lijalo la majira ya baridi ili kuondoka kwenye klabu ambayo imekuwa chungu kwake baada ya kutibuana na kocha Mdachi, Slot.