Slot kutembelea nyota ya ya Klopp Liverpool

Muktasari:

  • Kocha huyu Mjerumani anaamini ameiacha timu hiyo katika hali nzuri kwa kocha ajaye na timu ya vijana ambayo ilimsaidia kuchukua Carabao Cup Februari mwaka huu itasaidia zaidi kwenye kuijenga Liverpool mpya.

LIVERPOOL, ENGLAND: Jurgen Klopp amemtengenezea mazingira mrithi wake anayetajwa kuwa ni Arne Slot kwa kuwataka mashabiki kumwamini na kumpa muda ili aonyesha maajabu yake Anfield.

Kocha huyu Mjerumani anaamini ameiacha timu hiyo katika hali nzuri kwa kocha ajaye na timu ya vijana ambayo ilimsaidia kuchukua Carabao Cup Februari mwaka huu itasaidia zaidi kwenye kuijenga Liverpool mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari wikiendi iliyopita, Klopp alisema licha ya kuwa katika nafasi ya tatu kwa sasa anaamini wanaweza kupanda na kuwa hata mabingwa msimu ujao chini ya kocha mpya lakin itategemea na uwekezaji ambao mabosi wameufanya.

“Sio uamuzi wangu kumleta kocha mpya, na sipo hata katika nafasi ya kushauri, lakini nipo tayari kutoa ushirikiano kwa kocha mpya ikiwa itahitajika, dunia nzima ina namba yangu ya simu. Wanipigie tutazungumza kila kitu kinachoihusu Liverpool.”

“Nimewaachia moja kati ya vikosi bora, najua hii sio kazi yangu tena kupanga tunafanye vile au vipi, watakaokuja katika timu ndio watakuwa na wakati mzuri zaidi wa kuamua na kupanga’’

“Wataanza na kuangalia tulichofanya msimu huu jambo ambalo ni mwanzo mzuri, lakini pia wataangalia nani kutoka katika Akademi anafaa kupandishwa na kama kuna maboresho ya wachezaji wa nje wanaotakiwa kusajiliwa, hivyo ndo nafikiri wataenda kuanza navyo.

“Ukiangalia umri wa viungo wetu uavutia sana, mfano Stefan Bajcetic amerudi na kiwango chake nafikiri kinajulikana, baadhi ya wachezaji watatolewa kwa mkopo na wengine watauzwa, misingi ambayo tumeianzisha ni imara sana, tulijaribu kushinda Ligi Kuu England msimu huu lakini imeshindikana.”

Hata hivyo, Arne amesema ni kweli yupo katika mazungumzo na Liverpool lakini hadi sasa hawajafikia mwafaka kama inavyoelezwa na vyombo vingi vya habari.