Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot ashangaa PSG kuwafunga mawili tu

SLOT Pict

Muktasari:

  • Mabao ya Desire Doue na Khvicha Kvaratskhelia  yalitosha kuipa PSG, mabingwa watetezi wa Ulaya, ushindi ambao unaonekana ni faida kubwa wakati wanaelekea Anfield kwa ajili ya marudiano wiki ijayo.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot amekiri timu yake ilikuwa na bahati kutopoteza kwa mabao mengi zaidi dhidi ya Paris Saint-Germain baada ya kuchapwa 2-0 katika robo fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya katikati ya wiki hii.

Mabao ya Desire Doue na Khvicha Kvaratskhelia  yalitosha kuipa PSG, mabingwa watetezi wa Ulaya, ushindi ambao unaonekana ni faida kubwa wakati wanaelekea Anfield kwa ajili ya marudiano wiki ijayo.

Katika mechi hiyo, PSG ilipoteza nafasi nyingi za wazi mwishoni mwa mchezo ambazo zingeweza kuifanya Liverpool iwe katika hali mbaya zaidi.

Kipigo hicho kilikuwa ni cha 16 kwa Liverpool msimu huu katika mashindano yote, jambo linalowaacha na kazi ngumu ya kupindua matokeo hayo nyumbani.

Slot alikiri wazi timu yake ilizidiwa ubora huko Paris na ingeweza kufungwa mabao mengi zaidi ikiwa wapinzani wao wangekuwa makini.

"Ukiangalia mchezo mzima, nadhani tuna bahati kupoteza kwa mabao mawili tu. Lakini ni jambo zuri bado tupo kwenye ushindani, tunakutana nao Anfield na tunajua jinsi uwanja wetu unavyoweza kutupa  faida zaidi."

Kwa asilimia kubwa kipa wa majogoo Giorgi Mamardashvili alisaidia sana kupunguza idadi ya mabao akiokoa mipira hatari  ambayo ilionekana kuwa inaenda kuwa mabao.

Ousmane Dembele alikaribia kufunga bao la tatu mwishoni mwa mchezo, lakini mpira wake uligonga mwamba wa goli na kushindwa kuingia.

Slot alipanga kikosi chake kwa mfumo wa 5-3-2 ili kujaribu kuizuia PSG, lakini haikusaidia kwani walionekana kuwa weupe kuanzia nyuma hadi mbele kwenye kushambulia.

Alipoulizwa kama timu yake ilitengeneza nafasi za kutosha, Slot alijibu: "Ndiyo na hapana. Ndiyo kwa sababu tunataka kuunda nafasi nyingi zaidi, hapana kwa sababu haikuwa rahisi kupata nafasi. Tulijaribu mara nyingi kuwabana kwa juu, lakini walipenya kirahisi tulipocheza mtu kwa mtu."