Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Skendo! Mastaa 70 Serie A wachunguzwa biashara ya ngono

SKENDO Pict

Muktasari:

  • Uchunguzi huo umehusisha wachezaji kutoka klabu kubwa zikiwemo Inter Milan, AC Milan, Juventus, Hellas Verona, Torino, AC Monza na US Sassuolo, ingawa mamlaka zinasema hakuna mchezaji yeyote aliyefunguliwa mashitaka rasmi hadi sasa.

MILAN, ITALIA: Mvutano mkubwa umetanda katika soka la Italia baada ya takribani wachezaji 70 wa Ligi Kuu Italia (Serie A) kuhusishwa na uchunguzi wa mtandao wa ukahaba unaodaiwa kuendeshwa katika Jiji la Milan, katika operesheni inayoongozwa na Guardia di Finanza.

Uchunguzi huo umehusisha wachezaji kutoka klabu kubwa zikiwemo Inter Milan, AC Milan, Juventus, Hellas Verona, Torino, AC Monza na US Sassuolo, ingawa mamlaka zinasema hakuna mchezaji yeyote aliyefunguliwa mashitaka rasmi hadi sasa.

Guardia di Finanza, kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu wa kifedha na kiuchumi Italia, kimeeleza mtandao huo ulikuwa ukijificha kama wakala wa matukio ya burudani na sherehe za usiku, lakini kwa ndani ulikuwa ukiandaa huduma za ukahaba kwa wateja matajiri, wakiwemo baadhi ya wanamichezo wa kulipwa.

Katika taarifa za awali za uchunguzi, imeelezwa baadhi ya sherehe hizo zilihusisha matumizi ya gesi ya nitrous oxide, maarufu kama “laughing gas”, ambayo hutumika kubadilisha hali ya fahamu na kuleta hisia za furaha ya muda mfupi

SKE 02

. Wachunguzi wanasema hii ilitumika kama sehemu ya “burudani ya kifahari” katika matukio hayo.

Majina ya wachezaji hayakuwekwa wazi kwenye hati za mahakama, lakini vyombo vya habari vya Italia vimeorodhesha majina yanayodaiwa kutumika kwenye mawasiliano ya mtandao huo kama “wateja”, akiwemo Alessandro Bastoni, Raoul Bellanova, Achraf Hakimi, Philippe Coutinho, Milan Skriniar, Rafael Leão na Olivier Giroud.

Hata hivyo, mamlaka zinasisitiza uwepo wa majina hayo haumaanishi makosa ya jinai, kwani kwa mujibu wa sheria za Italia, wateja wa huduma hizo hawakuvunja sheria ikiwa hakuna ushahidi wa matumizi ya nguvu au uhalifu mwingine.

Msemaji wa uchunguzi alinukuliwa akisema: “Kwa bahati mbaya siyo kosa la jinai. Hakuna dalili ya vurugu. Wanawake walikubali kushiriki.”

SKE 01

Katika operesheni hiyo, watu wanne wamewekwa chini ya kifungo cha nyumbani kwa tuhuma za kuendesha mtandao wa ukahaba na utakatishaji wa fedha. Zaidi ya euro milioni 1.2 zimekamatwa, fedha ambazo zinadaiwa kuwa mapato haramu.

Uchunguzi unaendelea kuchambua mawasiliano ya simu na miamala ya kifedha, huku wakili wa baadhi ya watuhumiwa akipinga tuhuma hizo akidai ni “tafsiri potofu ya shughuli za burudani za kisheria”.

Kesi hiyo imezua mjadala mkubwa Italia kuhusu maisha binafsi ya wanamichezo na mipaka ya faragha, huku mashabiki wakisubiri majibu zaidi kutoka mahakama ya Milan.