Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simon Kalika aiacha hatima ya Super Eagle mikononi mwa Chelle

KALIKA Pict

Muktasari:

  • Nigeria leo Alhamisi Novemba 13, 2025 itacheza mechi ya mchujo ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Gabon, Gabon, itakayopigwa katika Uwanja wa Moulay Hassan, mjini Rabat, Morocco.

Kocha msaidizi wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria maarufu Super Eagles, Simon Kalika, amemtaka kocha mkuu wa sasa wa timu hiyo, Eric Chelle kuendelea na mikakati yeke sahihi, ili kuhakikisha anafanikisha mpango wa kulipeleka taifa hilo la Afrika ya Magharibi kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026.

Nigeria leo Alhamisi Novemba 13, 2025 itacheza mechi ya mchujo ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Gabon, Gabon, itakayopigwa katika Uwanja wa Moulay Hassan, mjini Rabat, Morocco.

Kalika amesema kuwa Super Eagles ina ubora wa kutosha kuibuka na ushindi dhidi ya timu ya Thierry Mouyouma, hivyo jukumu zito lililobaki ni kwa kocha Chelle kuchanga vizuri karata zake ndani ya dakika 90.

Mholanzi huyo amesema, anaamini kikosi cha Gabon kina uwezo wa kupambana, lakini sio mbele ya Nigeria yenye hamu ya mafanikio, tena ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia.

POS 02

“Ninajua wachezaji wanataka kwenda Kombe la Dunia. Nigeria ina ubora na uwezo. Ikiwa Shirikisho (NFF) na kocha watashirikiana ipasavyo, naamini Super Eagles inaweza kuwafunga Gabon 4-0 au 5-0,” Kalika ameambia Completesports.com.

Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia 2026, kati ya Nigeria dhidi ya Gabon imepangwa kuanza saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Mechi nyingine ya mchujo leo itakuwa kati ya Cameroon dhidi ya DR Congo itaanza saa 3:00 usiku, huku washindi wa mechi hizo mbili watakutana katika mechi itakayoamua mwakilishi wa Afrika atakayeendelea na mchakato wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026.