Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shughuli ya EPL kuendelea wikiendi hii, Chelsea v Liverpool

LIGI Pict

Muktasari:

  • Mechi kubwa zaidi itakuwa kati ya Chelsea na Liverpool itakayopigwa Stamford Brifge kuanzia saa 1:30 usiku ambapo kwa Liverpool itakuwa ni nafasi ya kurejea katika mstari baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo.

LONDON, ENGLAND: HEKAHEKA za Ligi Kuu England zitaendelea wikiendi hii ambapo mechi nne ambazo zinasubiriwa kwa hamu kwani huenda zikaamua timu ipi itakuwa kuleleni wiki mbili zijazo.

Mechi kubwa zaidi itakuwa kati ya Chelsea na Liverpool itakayopigwa Stamford Brifge kuanzia saa 1:30 usiku ambapo kwa Liverpool itakuwa ni nafasi ya kurejea katika mstari baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo.

Vilevile inataka sana kupata matokeo katika mechi hiyo kwani ikiwa itapoteza au kutoka sare kuna asilimia kubwa ya kushushwa na Arsenal.

Timu hizo ziliwahi kukutana katika mechi 199 za michuano yote Chelsea ikishinda 66, kupoteza 87 huku 46 ikiwa sare.

Kabla ya msimu uliopita Chelsea haikuwa imepata ushindi katika mechi 10 mbele ya Liverpool kwenye michuano yote, lakini mwiko huo ulivunjwa baada ya Enzo Maresca kushinda 3-1 dhidi ya mabingwa hao watetezi.

Jambo baya kwa Liverpool ni kwamba itakuwa inamkosa kipa tegemeo Allison Becker ambaye atakuwa nje kwa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na tatizo la za paja. Kwa Chelsea itamkosa beki Trevoh Chalobah aliyeonyeshwa kadi nyekundu wikiendi iliyopita dhidi ya Brighton.

Chelsea imekuwa ikiandamwa na kadi nyekundu ambazo katika mechi nne  zilizopita wachezaji watatu wameonyeshwa na kwa kiasi kikubwa ziliiathiri kwani tatu kati ya hizo ilipoteza na moja dhidi ya Benfica katika Ligi ya Mabingwa ilishinda.

Liverpool inaongoza ligi ikiwa na pointi 15 na Arsenal inafuatia na 13, hivyo mechi hiyo ikitoka sare na Arsenal ikashinda itakuwa imeifikia na huenda ikashushwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Arsenal ambayo haijapoteza mechi katika michuano yote tangu ipoteze Ligi Kuu England Agosti Mosi dhidi ya Liverpool itakuwa nyumbani kucheza na West Ham.

LIG 03

Katika Mechi hiyo itakayoanza saa 11:00 jioni Arsenal inapewa nafasi kubwa zaidi ya kupata matokeo mazuri tofauti na West Ham ambayo tangu kuanza kwa msimu imekuwa na wakati mgumu.

Kwa sasa vijana hao wa London wapo nafasi mbaya (19) wakiwa wamekusanya alama nne katika mechi sita, wakishinda moja na sare moja. Hata hivyo, licha ya kiwango cha sasa historia inaonyesha West Ham si vibonde kwa Arsenal na katika mechi tano za mwisho za Ligi Kuu England, moja ilimalizika kwa sare kisha nne Arsenal ilishinda mbili na West Ham mbili.

Manchester United ya Ruben Amorim kesho itakuwa kibaruani itakapoikaribisha Sunderland.Mashetani Wekundu ambao wameshinda mechi mbili kati ya sita za ligi msimu huu watakutana na Sunderland ambayo licha ya kupanda daraja imeonekana kuwa moto mkali.

LIG 01

Sunderland ambayo ilisajili majina makubwa kama Granit Xhaka dirisha lililopita la majira ya kiangazi kwa sasa inashika nafasi ya tano baada ya kushinda mechi tatu sare mbili na kufungwa moja.

Kikosi hicho kinachonolewa na Mfaransa Regis Le Bris mechi pekee ambayo kimepoteza ni dhidi ya Burnley lakini baada ya hapo kimepata alama mbele ya timu zote kilizokutana nazo ikiwemo Liverpool na Crystal Palace.

Ikiwa Man United itapoteza mechi hiyo huenda ajira ya Amorim ikawa shakani zaidi katika kipindi hiki ambacho mashabiki wengi wanataka afukuzwe ingawameendelea kusisitiza kuwa hajali na hatabadilika. Man United kwa sasa inashika nafasi ya 14 ikiwa na pointi saba.

LIG 02

Mechi ya mapema zaidi kwa leo itapigwa viungani Elland Road ambapo Tottenham Hotspur itakaribishwa na Leeds United saa 8:30 mchana.

Licha ya kuanza vizuri msimu huu karibuni Spurs imekuwa ikipitia wakati mgumu na imeambulia sare katika mechi mbili mfululizo za ligi.

Mechi ya wikiendi iliyopita ndio iliwachefua zaidi mashabiki baada ya kutoka sare dhidi ya Wolves ambayo haikuwa imepata pointi yoyote katika mechi tano na ilikuwa inaburuza mkia katika msimamo.

Spurs ipo nafasi ya nne katika msimamo lakini ikipoteza mechi hii inaweza kujikuta saba wakati Leeds ikishinda inaweza ikasogea hadi nafasi ya tano.