Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot: Huyu Isak kuna kitu bado

SLOT Pict

Muktasari:

  • Straika huyo aliyesajiliwa kwa Pauni 130 milioni kutoka Newcastle United, aliwekwa kando kwenye kikosi cha Liverpool kilichopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burnley kwenye Ligi Kuu England, hayupo kwenye ufiti wa kutosha wa kucheza mechi baada ya kutumika kwa dakika 18 tu kwenye mechi za kimataifa alipoitumikia Sweden.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA Mkuu wa Liverpool, Arne Slot amekiri mchezaji ghali Uingereza, Alexander Isak hayupo kwenye viwango vya kutosha kuanzishwa kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Straika huyo aliyesajiliwa kwa Pauni 130 milioni kutoka Newcastle United, aliwekwa kando kwenye kikosi cha Liverpool kilichopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burnley kwenye Ligi Kuu England, hayupo kwenye ufiti wa kutosha wa kucheza mechi baada ya kutumika kwa dakika 18 tu kwenye mechi za kimataifa alipoitumikia Sweden.

Isak hakufanya mazoezi ya pre-season na timu yake ya Newcastle baada ya kugomea akilazimisha uhamisho wake wa kwenda kujiunga na miamba ya Anfield dirisha lililopita.

Straika huyo alikuwa na vipindi vya mazoezi magumu Jumamosi iliyopita wakati wenzake walikuwa huko Turf Moor kusaka ushindi wao wa nne wa EPL msimu huu na ulipatikana kwa bao la mkwaju wa penalti la Mohamed Salah dakika za majeruhi.

“Kama unaanza msimu na wachezaji waliokuwa mapumziko kwa wiki tano, utahitaji kuwatengenezea msingi mzuri kabla ya kuanza kumtumia kwa dakika 45,” alisema Slot, ambaye kikosi chake kitamenyana na Atletico Madrid kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, usiku wa Jumatano.

“Tulimchukua Newcastle ambako hakuwa na pre-season, hivyo anahitaji dakika kadhaa za kufanya mazoezi ili kupata msingi unaohitajika, kabla ya kuanza kucheza. Alex bado hayupo tayari kuanza kucheza, lakini anaweza kutumika kwa dakika tano au 10 Ligi ya Mabingwa Ulaya.”