Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shughuli ya Carabao Cup kuendelea leo

SHUGHULI Pict

Muktasari:

  • Leo kutakuwa na jumla ya mechi nane lakini zile zinazotarajiwa kufuatiliwa na mashabiki wengi zaidi ni ile Chelsea itakayokuwa ugenini dhidi ya Lincoln City kuanzia saa 3:45 usiku pamoja na Liverpool dhidi ya Southampton itakayoanza saa 4:00 usiku.

LONDON, ENGLAND: BAADA ya mechi za raundi ya tatu za michuano ya Kombe la Carabao kuanza wiki iliyopita, vigogo wawili wa timu sita kubwa za England zitashuka dimbani leo katika mechi za raundi hiyo zitakazopigwa wiki hii na ijayo.

Leo kutakuwa na jumla ya mechi nane lakini zile zinazotarajiwa kufuatiliwa na mashabiki wengi zaidi ni ile Chelsea itakayokuwa ugenini dhidi ya Lincoln City kuanzia saa 3:45 usiku pamoja na Liverpool dhidi ya Southampton itakayoanza saa 4:00 usiku.

Liverpool ambayo msimu uliopita ilifika fainali na kupoteza mbele ya Newcastle itakuwa inahitaji kuendeleza ubabe wa kushinda mechi saba mfululizo za michuano yote baada ya sasa kuwa imeshinda tano za Ligi Kuu England na moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Majogoo hao wanatarajiwa kupumzisha baadhi ya wachezaji wao muhimu akiwemo Mohamed Salah, Virgil van Dijk na Ibrahim Konate ambao walicheza mechi tatu zilizopita na kumaliza dakika zote 90.

Mbali na  mechi hii itakayopigwa katika dimba la Anfield kule Lincoln kwenye Uwanja wa LNER, Chelsea itakuwa inaumana na Lincoln FC inayocheza Ligi Daraja la Pili.

Uwanja utakaotumika kwa ajili ya mchezo huo ni mdogo sana ukilinganisha na viwanja ambavyo Chelsea imezoea kucheza. Uwanja huo una uwezo wa kuchukua jumla ya mashabiki 10,000.

Chelsea ambayo imeanza msimu vizuri baada ya kushinda ubingwa wa Kombe la Dunia kwa klabu bado inahitaji kushinda mechi hii ili kupunguza presha kutokana na matokeo mabovu ambayo imeyapata hivi karibuni ikiwemo kufungwa na Manchester United mabao 2-1.

Timu nyingine za EPL pia zitashuka dimbani leo, Wolves ikiwa nyumbani itavaana na Everton, Fulham pia itakuwa nyumbani kuikaribisha Cambridge, Brighton itasafiri kuifuata Barnsley wakati Burnley ikiikaribisha Cardiff City ambapo mechi zote zinatarajiwa kuanza saa 3:45 usiku.

Mechi nyingine ni Wrexham timu ambayo inaonekana kuja kwa kasi ikiwa inasumbua katika Ligi Daraja la kwanza England itakuwa nyumbani kuikaribisha Reading huku Wycombe ikisafiri hadi Wigan kuvaana na Wigan Athletic.