Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shearer: Isak? Amekosea kwenda Liverpool

Muktasari:

  • Isak alianzisha hadi mgomo huko Newcastle United wakati analazimisha uhamisho wa kwenda Liverpool jambo ambalo lilitimia katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa majira ya kiangazi.

NEWCASTLE, ENGLAND: GWIJI wa Ligi Kuu England, Alan Shearer amesema straika Alexander Isak hajajitendea haki kwa uamuzi wake wa kwenda kujiunga na Liverpool.

Isak alianzisha hadi mgomo huko Newcastle United wakati analazimisha uhamisho wa kwenda Liverpool jambo ambalo lilitimia katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa majira ya kiangazi.

Shearer alisema: "Haukuwa mwanzo mzuri wa msimu ambao Isak angependa kuanza nao. Unapofikiria fowadi ya Sweden yenye washambuliaji Gyokeres, Isak na Elanga na bado hawafungi mabao wakiifanya timu yao ya taifa kuwa kwenye hatihati ya kufuzu Kombe la Dunia.

"Kocha amekumbwa na tatizo na kupoteza kibarua chake. Ni hicho pia kilichotokea Newcastle, Isak hakucheza wala kufanya mazeozi na hafanyi vizuri Liverpool, alihitaji kurudi kwenye ubora wake katika mechi za kimataifa, lakini mambo yamekuwa kinyume.

"Mambo hayaendi, hakufunga na wenzake hawakufunga pia. Ukitazama ile fowadi ya Sweden na bado timu inashika nafasi ya chini kwenye kundi lao, sio vizuri kabisa. Hiki kipindi cha majira ya kiangazi, Isak hajajitendea haki kabisa."