Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Semenyo kupimwa afya Etihad kesho

SEMENYO Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana amepangiwa kufanya vipimo vya afya siku ya Alhamisi, huku dili lake la Pauni 65 milioni kwenda Etihad likitarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa wiki.

LONDON, ENGLAND: WINGA, Antoine Semenyo anatarajia kukamilisha uhamisho wake kwenda Manchester City baada ya kuichezea Bournemouth mara ya mwisho Jumatano usiku.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana amepangiwa kufanya vipimo vya afya siku ya Alhamisi, huku dili lake la Pauni 65 milioni kwenda Etihad likitarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa wiki.

Man City ilikubali kuamsha kifungu cha kuvunja mkataba ili kumsajili mchezaji huyo wa zamani wa Bristol City katika siku za mwisho za mwaka 2025.

Hata hivyo, Man City waliridhia Bournemouth kumtumia katika mechi tatu zilizo karibu na kipindi cha Mwaka Mpya.

Hivyo basi, ujio wa Tottenham katika Uwanja wa Vitality, usiku wa Jumatano, siku ambayo Semenyo anatimiza miaka 26, ulionekana kuwa mechi yake ya kuaga klabu hiyo ya Pwani ya Kusini.

Kocha wa Bournemouth, Andoni Iraola, amesema: “Antoine atacheza kesho (Jumatano). Ukiniuliza mimi binafsi, nadhani inaweza kuwa mechi yake ya mwisho. Lakini bado hakuna kilichokubaliwa rasmi, wala kusainiwa.”

SEME 01
SEME 01

Man United pia walikuwa na nia ya kumsajili Semenyo, lakini fursa ya kufanya kazi chini ya Pep Guardiola na kushindania mataji ilibeba uzito mkubwa katika uamuzi wake. Iwapo mambo yataenda kama ilivyopangwa, Semenyo anaweza kuichezea Man City kwa mara ya kwanza katika raundi ya tatu ya Kombe la FA dhidi ya Exeter City ya League One, mechi itakayopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Etihad.

Kuondoka kwake Bournemouth kutakuwa pigo kubwa katika nguvu yao ya ushambuliaji. Semenyo amefunga mabao tisa katika mechi 19 za Ligi Kuu msimu huu, na ndiye mfungaji bora wa klabu hiyo. Kocha Iraola aliongeza katika mahojiano na vyombo vya habari kwamba mshambuliaji huyo ni “karibu haiwezekani kumpata mbadala wake.”

Uhamisho wa Semenyo kwenda Man City utamfanya ajiunge na safu imara ya ushambuliaji inayomjumuisha nyota mkubwa kama Erling Haaland.

Man City bado inapambana katika mashindano manne kwa wakati mmoja, yakiwamo mashindano matatu ya ndani: Ligi Kuu, Kombe la FA na Kombe la EFL.

Pia wana majukumu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakiwa na mechi mbili za mwisho za hatua ya ligi zitakazochezwa mwezi huu dhidi ya Bodo/Glimt na Galatasaray. Kwa sasa, kikosi cha Pep Guardiola kinashika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kiko katika mwelekeo mzuri wa kumaliza ndani ya nane bora, jambo litakalowapa tiketi ya moja kwa moja ya kufuzu hatua ya 16 bora.