Schmeichel asepa Leicester City

Thursday August 04 2022
ester pic

LONDON, ENGLAND. KASPER Schmeichel amekamilisha uhamisho wa kujiunga na Nice kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kuondoka Leicester City.
Schemichel ametengeneza historia Leicester akidumu kwa muda wa miaka 11, akiisaidia klabu hiyo kubeba ubingwa wa Kombe la FA mwaka mwaka jana pamoja na Kombe la Ligi Kuu England mwaka 2016.
Kipa huyo wa Kimataifa wa Denmark alijiunga na Leicester tangu mwaka 2011, aliposajiliwa kwa kitita cha Pauni 5.1 milioni
Kuondoka kwa Schmeichel inampa Danny Wards nafasi ya kuwa kipa namba moja katika kikosi cha kwanza cha Leicester.
Mwenyekiti wa klabu hiyo  Aiyawatt Srivaddhanaprabha amesema Schmeichel ni mchezaji aliyekuwa akijituma kutokana na mchango wake miaka yote aliyokuwepo hapa.
“Alikuwa kiongozi nje na ndani ya uwanja, kipindi chote alichokuwepo na sisi, Kasper aliiongoza timu kwa ueledi kama nahodha wetu miaka yote,” alisema Mwenyekiti huyo.


Advertisement