Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sancho afichua siri ya Marcesa

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa Sancho ambaye alikuwa mchezaji muhimu katika mchezo huo akitoa asisti ya bao la kuongoza la Chelsea akimpasia Cole Palmer kabla ya Palace kusawazisha kupitia Jean Philippe Mateta aliyefunga dakika za jioni, kocha aliwaambia kwamba mechi ilitakiwa kuisha mapema.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Chelsea, Enzo Maresca amewaambia wachezaji wake kwamba wajifunze kumaliza mechi mapema baada ya kuwaachia Crystal Palace nafasi ya kurudisha bao na kufanya mchezo umalizike kwa sare wikiendi iliyopita, amefichua Jadon Sancho.

Kwa mujibu wa Sancho ambaye alikuwa mchezaji muhimu katika mchezo huo akitoa asisti ya bao la kuongoza la Chelsea akimpasia Cole Palmer kabla ya Palace kusawazisha kupitia Jean Philippe Mateta aliyefunga dakika za jioni, kocha aliwaambia kwamba mechi ilitakiwa kuisha mapema.

Baada ya sare hiyo, Chelsea sasa inakuwa imecheza mechi nne mfululizo bila ya kupata ushindi hali inayowaweka katika nafasi mbaya katika harakati zao za kuwania ubingwa na nafasi nne za juu.

Akizungumza na BBC Radio 5 Live, Sancho alisema: “Nadhani tulicheza vizuri na kudhibiti mchezo kwa kiasi kikubwa, hivyo ilikuwa ni jambo la kuhuzunisha sana kuruhusu bao la mwishoni. Kama vile kocha alivyosema kwenye chumba cha kubadilishia nguo, lazima tuwe tunamaliza mechi mapema.”

“Nadhani kama tungefunga bao la pili, tungekuwa na utulivu zaidi na wao wangefunguka zaidi, jambo ambalo lingeweza kutufungulia nafasi ya kufunga mabao mengine, lazima tujifunze kutokana na hili na kusonga mbele,” aliongeza Sancho.

“Ni lazima tufanye vyema katika kumalizia nafasi zetu. Bado tulitengeneza  nafasi nyingi mbele ya lango, lakini hazikuwa na maana kwa sababu hatukuzitumia, mimi naona bado tunacheza soka lile lile (kama ilivyokuwa kwa wiki zilizopita), bado tunajitoa kwa asilimia 100. “

Licha ya kuanza vizuri ligi, Chelsea ilimaliza mwaka 2024 kwa matokeo mabaya baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Fulham na Ipswich Town.  “Katika  kipindi cha kwanza na cha pili, tulitengeneza nafasi za kutosha kutupa ushindi.”