Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sakata mkataba mpya wa Bruno Man United

Muktasari:

  • Nahodha huyo wa Man United ana mkataba hadi mwaka 2028, lakini anaweza kuondoka Old Trafford katika dirisha la majira ya kiangazi.

MANCHESTER, ENGLAND: KIUNGO wa boli, Bruno Fernandes hatatafuta uhakika wa kuhusu usajili wa mastaa wake kwenye kikosi cha Manchester United kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi kabla ya kuamua mustakabali wake.

Nahodha huyo wa Man United ana mkataba hadi mwaka 2028, lakini anaweza kuondoka Old Trafford katika dirisha la majira ya kiangazi.

Mmiliki mwenza wa klabu hiyo, bilionea Jim Ratcliffe, pamoja na viongozi wengine wakuu wanatamani kumbakiza Fernandes na wanataka aongeze mkataba wake.

Klabu hiyo tayari imeweka wazi msimamo wake kwa nyota huyo wa kimataifa wa Ureno, ikiwa tayari kumpa mkataba mpya ulioboreshwa wenye thamani ya hadi Pauni 400,000 kwa wiki.

Fernandes, ambaye atatimiza miaka 32 Septemba, anatambua kuwa mkataba wake ujao huenda ukawa wa mwisho katika taaluma yake. Anataka kuhakikisha kuwa matarajio ya Man United yanaendana na yake linapokuja suala la kushinda mataji makubwa.

Hata hivyo, licha ya ushawishi wake mkubwa kwenye klabu kama nahodha, Fernandes hatadai kujua ni wachezaji gani viongozi wa klabu wanapanga kusajili.

Man United imekuwa ikihusishwa na majina ya viungo kama Elliot Anderson, Adam Wharton, Sandro Tonali na Bruno Guimaraes katika mipango yao ya kuboresha safu ya kiungo kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Inaelezwa kwamba Fernandes ataegemeza uamuzi wake juu ya kama Man United itafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao au la. Pia anataka kuona kama klabu itaamua kumthibitisha Michael Carrick kama kocha wa kudumu. Fernandes amevutiwa na athari chanya aliyoleta Carrick tangu alipochukua mikoba kwa muda na amekuwa akielewana naye vyema.