Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saka: Arsenal kila siku inaonewa

SAKA Pict

Muktasari:

  • Mwamuzi Jarred Gillett awali aliamua ilikuwa ni penalti, lakini baada ya muda akaenda kutazama katika  VAR na alibadilisha uamuzi wake.

LONDON, ENGLAND: STAA wa Arsenal, Bukayo Saka ametoa maneno makali dhidi ya VAR baada ya Arsenal kunyimwa penalti kipindi cha kwanza, licha ya faulo ambayo straika wao, Viktor Gyokeres alifanyiwa na kipa wa Newcastle United, Nick Pope.

Mwamuzi Jarred Gillett awali aliamua ilikuwa ni penalti, lakini baada ya muda akaenda kutazama katika  VAR na alibadilisha uamuzi wake.

Hata hivyo, Arsenal bado iliibuka na ushindi wa  mabao 2-1 kwa bao la dakika za mwisho lililofungwa na Gabriel, lakini Saka alionyesha kutoridhishwa kwake na uamuzi wa kubatilisha penalti ya kipindi cha kwanza.

Katika mahojiano yake baada ya mechi, Saka alidai maamuzi ya aina hii kila mara huwa yanatokea kuwaumiza wao.

SAK 01

Marudio ya picha yalionyesha Pope alipiga mpira kidogo kabla ya kumwangusha Gyokeres jambo ambalo lilimwaminisha mwamuzi kuwa kipa huyo hakufanya faulo.

Hata hivyo, Arsenal inaamini mgusano uliotokea kati ya Pope na Gyokeres ulimyima mshambuliaji huyo nafasi ya kufunga bao jambo ilipaswa kumfanya mwamuzi aamue ilikuwa ni penalti.

Saka, aliyerejea kikosini baada ya kuwa nje kwa muda kutokana majeraha, aliisaidia Arsenal kubadilika kiuchezaji hata ikasawazisha na kuongeza bao la ushindi.

SAK 02

Ushindi huo uliipandisha Arsenal hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, ikiwa pointi mbili tu nyuma ya Liverpool, ambayo ilipoteza dhidi ya Crystal Palace Jumamosi.

"Ni mambo kama haya ambayo kila mara huwa yanatokea na kuyunyima nafasi, lakini leo tumepata tulichostahili na ndiyo maana wote tuna furaha. Sasa haijalishi tena ikiwa tulinyima penalti."