Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal wana jambo lao... Acha wapinzani waone wivu!

back Pict

Muktasari:

  • Lakini, swali linaloulizwa ni kama safu hiyo mpya ya ushambuliaji iliyotengenezwa na kocha Arteta itaweza kumaliza ukame wa taji la Ligi Kuu England msimu huu na kuhakikisha linatua Emirates.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amekusanya safu matata ya ushambuliaji inayofanya wapinzani wao kwenye Ligi Kuu England waone wivu, wakitamani wachezaji hao wawepo kwenye vikosi vyao.

Lakini, swali linaloulizwa ni kama safu hiyo mpya ya ushambuliaji iliyotengenezwa na kocha Arteta itaweza kumaliza ukame wa taji la Ligi Kuu England msimu huu na kuhakikisha linatua Emirates.

Mchana wa jana Jumamosi, chama hilo lilijimwaga huko Emirates kukabiliana na Nottingham Forest kwenye mchezo matata kabisa wa Ligi Kuu England. Kilichotokea, kimetokea. Ndiyo kama mlivyosikia.

Baada ya misimu kadhaa ya kupiga hatua moja baada ya nyingine, hatimaye, Arsenal iliamua kufunga kazi kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi kwa kunasa huduma za wachezaji matata kabisa katika eneo la ushambuliaji, ili mabao yafungwe, mataji yanaswe.

Usajili wa straika la mabao, Viktor Gyokeres, winga wa boli, Noni Madueke, na kiungo fundi wa mpira mwenye ubunifu mwingi, Eberechi Eze yanakifanya kikosi hicho cha Arteta kuwa na uwezo wa kupenya ngome yoyote ile ya mabeki wa timu pinzani na kufanya maangamizi.

Msimu uliopita, mbio zao kwenye kusaka ubingwa wa Ligi Kuu England zilikwama mwishoni baada ya wachezaji wake muhimu kwenye safu ya ushambuliaji kupata majeraha, akiwamo Mjerumani, Kai Havertz.

Gabriel Jesus naye aliumia na kufanya mabao kuwa adimu kwenye kikosi hicho. Lakini, sasa ujio wa straika wa Pauni 64 milioni, Gyokeres, aliyenaswa kutoka Sporting Lisbon, amekuja kumaliza tatizo la mabao.

Straika huyo wa kimataifa wa Sweden, ni Namba 9 wa kiwango cha juu, akimiliki vitu vyote muhimu, nguvu, ubunifu na uwezo wa kupachika mpira kwenye nyavu za wapinzani.

Mchango wake kwenye timu utahitajika kupatikana haraka, hasa ikingatiwa atawekwa mbele kabisa kwenye safu ya ushambuliaji huku kipaumbele chake kikiwa kweye kuweka mipira kwenye nyavu. 

Arteta pia alimsajili Madueke kwa Pauni 52 milioni kutoka kwa mahasimu wao wa Ligi Kuu England, Chelsea na Eze kutoka kwa wapinzani wao wengine wa London, Crystal Palace kwa ada ya Pauni 67.5 milioni, ambao wanafanya safu hiyo ya ushambuliaji ya Arsenal kuwa isiyotabirika. 

Mastaa hao watatu wapya wanakuja kuongeza upinzani wa namba katika kikosi hicho cha Emirates. Bukayo Saka, ndiye anaonekana kuwa na nafasi kwenye vita hiyo, jambo ambalo litamfanya Arteta kukuna kichwa jinsi ya kuamua nani wa kuanza kwa kulingana na mpinzani.

Bila shaka mastaa kama Havertz, Gabriel Martinelli na Jesus watakuwa kwenye wakati mgumu zaidi wa kupata nafasi ya kuanza kikosini sawa na itakavyokuwa kwa Leandro Trossard, mwenye uwezo wa kucheza kwenye maeneo mengi katika safu ya ushambuliaji.

Arteta ana machaguo mengi sana kwenye safu yake ya ushambuliaji na hilo ndilo linalomfanya kocha huyo kuwa na nguvu ya kupambana na wapinzani makini kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.

Gyokeres tayari ana uhakika wa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Arteta, huku kocha huyo Mhispaniola atakuwa na kazi ya kutafuta namna bora ya kupata huduma ya kweli kwa mastaa Madueke na Eze.

Alipokuwa Palace, Eze alikuwa anacheza zaidi kama Namba 10, lakini ana uwezo pia wa kushambulia kutokea kushoto. Staili yake ya uchezaji ni tofauti na ile ya Saka, ambaye hutokea kulia.

Madueke naye ameshaonyesha kitu kwa mechi tatu alizocheza kwenye kikosi hicho cha Arsenal, ni winga matata kabisa mwenye ubunifu mkubwa.