Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saka akimbizana kuwahi Man City

SAKA Pict

Muktasari:

  • Winga huyo wa Arsenal alikumbana na maumivu ya misuli dakika 53 katika mchezo wa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Leeds United kwenye Ligi Kuu England uwanjani Emirates, Jumapili iliyopita.

LONDON, ENGLAND: BUKAYO Saka anakimbizana na muda ili kupona haraka kwa ajili ya kulitumikia chama lake la Arsenal kwenye mechi ya kibabe dhidi ya Manchester City, mwezi ujao.

Winga huyo wa Arsenal alikumbana na maumivu ya misuli dakika 53 katika mchezo wa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Leeds United kwenye Ligi Kuu England uwanjani Emirates, Jumapili iliyopita.

Kocha Mikel Arteta alisema baada ya mechi: “Alihisi maumivu wakati anakimbia. Ile haikuwa ishara nzuri. Lakini, aliwahi kuwa na aina hii ya maumivu huko nyuma. Anafahamu hakika hali ilivyo.”

Arteta alifichua pia ni misimu ya upande mwingine wa ule ambao Saka ylimkabili kwenye mechi dhidi ya Crystal Palace, Desemba mwaka jana na hivyo kukaa nje kwa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji.

Kinachoelezwa ni kwamba matumaini ya majeraha hayo si makubwa, lakini Saka anatazamiwa kuwa nje ya uwanja kati ya wiki tatu hadi nne.

Hiyo ina maana, atakosa mechi ya Jumapili dhidi ya Liverpool huko Anfield na hatakuwapo kwenye mechi ya England dhidi ya Andorra, Septemba 6 na ile dhidi ya Serbia, Septemba 9.

Arsenal itacheza na Nottingham Forest, Septemba 13, lakini kocha Arteta atatamani Saka awe fiti kwa ajili ya mechi ya Man City, Septemba 21.

Mapumziko ya mechi za kimataifa kitakuwa kipindi kizuri kwa Saka kupona majeraha yake.