Rudiger kusalia Chelsea

Thursday January 13 2022
chelsea pic

WAKATI mazungumzo baina ya wawakilishi wa beki kisiki wa Chelsea  na Ujerumani, Antonio Rudiger na wawakilishi wa PSG na Real Madrid kuendelea na kuripotiwa kwamba yapo kwenye hatua nzuri, taarifa zinadai dili la staa huyo kuondoka Chelsea linazidi kuwa  na ufinyu wa kufanikiwa kwa sababu staa huyo ameonyesha nia ya kuendelea kusalia Chelsea.
Rudiger ambaye ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Chelsea amegoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Chelsea kwa sababu anahitaji mshahahara mrefu zaidi.
Lakini Chelsea imeonekana kuwa na ugumu wa kukubali kumpa ofa ya mshahara anayohitaji jambo linalosababisha fundi huyo achelewe kuongeza mkataba.
Hata hivyo, Rudiger hana haraka na bado ameendelea kuwapa mabosi wa  Chelsea kujadili na kumpa ofa nono ya mshahara kwenye ofa yao ya mkataba mpya.

Advertisement