Rudiger akabidhiwa jezi ya Isco, Alonso Madrid

Monday June 20 2022
Rudi PIC

MADRID, HISPANIA. MABINGWA wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na La Liga Real Madrid imemtambulisha rasmi beki Antonio Rudiger na kukabidhiwa jezi yenye namba 22 mgongoni.
Jezi hiyo iliwahi kuvaliwa na mastaa wa timu hiyo kama Isco Alcaron, Xabi Alonso na Paco Pawan ambao hawapo katika klabu hiyo kwasasa.
Rudiger ametabulishwa kama mchezaji rasmi wa Real Madrid, akitokea Chelsea na amesaini mkataba wa miaka minne, kukipiga Santiago Bernabeu msimu ujao.
Akizungumza baada ya utambulisho huo Rudiger amesema anajisikia furaha kujiunga na Real Madrid, Mabingwa wa Ligi Mabingwa Ulaya msimu uliyopita.
“Hii ni siku kubwa kwangu, napenda kuwashukuru wazazi wangu, bila ya uwepo wao nisingekuwa hapa, walinipa sapoti siku zote, wamekuwa muhimu katika maisha yangu, napenda kumpa shukrani za dhati Rais wa klabu, Florentino Perez kwa nafasi aliyonipa,” alisema Rudiger.

Advertisement