Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo asepa Saudia, aenda Hispania akikwepa mabomu ya Iran

Muktasari:

  • Ronaldo (41), ambaye anaishi Riyadh pamoja na mpenzi wake Georgina Rodriguez na watoto wao watano, yupo Saudi Arabia tangu alipojiunga na klabu ya Al-Nassr.

RIYADH, SAUDI ARABIA: NDEGE ya kifahari ya supastaa Cristiano Ronaldo imeonekana ikipaa kuondoka Saudi Arabia usiku mkubwa wakati mabomu ya Iran yaliyolenga kwenye ubalozi wa Marekani katika jijini la Riyadh yakianguka kama mvua.

Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 41 anaishi katika mji mkuu huo wa Saudi Arabia na mpenzi wake, mrembo Georgina Rodríguez pamoja na watoto wake watano, lakini haijafahamika kama walikuwa ndani ya ndege hiyo yenye thamani ya Pauni 61 milioni kwa usiku huo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya Iran, mashambulizi mawili ya ndege zisizo na rubani yalilenga makao ya kidiplomasia ya Marekani nchini humo usiku kucha. Iran pia ilitangaza kuwa jengo la wafanyakazi nchini Bahrain liliharibiwa.

Raia wa kigeni wanaripotiwa kuondoka Mashariki ya Kati kwa maelfu huku mzozo huo wa umwagaji damu ukiingia siku ya nne.

Hii inajiri wakati aliyekuwa mchezaji mwenzake Ronaldo katika kikosi cha Manchester United, Rio Ferdinand, alikiri alikuwa na hofu baada ya mashambulizi ya makombora yaliyowalazimu familia yake kujifungia nyumbani kama ilivyokuwa kipindi cha Uviko 19, wakati huu akiwa Dubai.

Taarifa za ufuatiliaji wa ndege zilionyesha ndege ya Bombardier Global Express ya supastaa huyo wa soka ilisafiri kwa takriban saa saba kuelekea mji mkuu wa Hispania huko Madrid. Ndege hiyo iliondoka saa mbili usiku na kutua karibu saa saba usiku.

Tovuti ya Flightradar24 inaonyesha ndege ya nyota huyo wa Ureno ilipita juu ya Misri na kuvuka Bahari ya Mediterania kabla ya kutua Madrid. Ronaldo alinunua ndege hiyo ya kisasa kwa Pauni 61 milioni mwaka 2024 baada ya kuuza ndege nyingine aina ya Gulfstream G200 aliyoinunua kwa Pauni 16 milioni 2015.

Ndege hiyo nyeusi maridadi inaweza kubeba abiria 15 na ina vyumba mbalimbali, ikiwemo chumba cha kulala chenye kitanda cha watu wawili na eneo tofauti la kuogea. Imewekwa nembo ya mchezaji huyo kila sehemu na ina picha ya ushangiliaji wake maarufu.

Mrembo  Georgina Rodríguez alitumia ndege hiyo wakati aliposafiri kwenda Milan wiki iliyopita.

Rafiki wa zamani wa Ronaldo, Ferdinand, 41, amelazimika kujihifadhi katika chumba cha chini ya ardhi huko Dubai kutokana na mawimbi ya mashambulizi ya Iran. Raia huyo wa Uingereza anaishi UAE pamoja na mkewe Kate, 34, na watoto wao Cree, mwenye miaka mitano, na Shae, mwenye miaka miwili, pamoja na binti wa Rio aitwaye Tia, 14. Watoto wake, Lorenz, 19, na Tate, 17, hawakuhamia walipohama kutoka Uingereza mwaka jana ili kuzingatia taaluma zao za soka.

Mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yalisababisha mashambulizi ya kulipiza kisasi katika maeneo mbalimbali ya ukanda huo, yakiwemo Falme za Kiarab.

Akizungumza katika kipindi chake Rio Ferdinand Presents, beki huyo wa zamani wa Man United na England alisema: “Wiki hii imekuwa tofauti kwangu, siwezi kuficha. Kwanza kabisa, niko katika hali nzuri asubuhi hii kwani familia nzima tulifanya mazoezi. Kama ilivyokuwa kipindi cha uviko, familia nzima tunafanya mambo ambayo kwa kawaida hatungefanya pamoja. Tunaendesha masomo ya nyumbani leo kidogo.

“Inatisha unaposikia makombora, ndege na ndege za kivita sijui hasa ni nini zikipita juu yetu na unasikia milipuko mikubwa, lakini hatujui kwa undani ni nini hasa kinachoendelea. Ni kuwaeleza watoto wako hali halisi na kuwasaidia kupitia kipindi hiki, jambo ambalo ni muhimu hasa kama baba wa familia. Unataka kubaki mtulivu na kuhakikisha kila mtu anabaki mtulivu kadri inavyowezekana.”

Ferdinand aliongeza: “Kwa kweli, imekuwa hali ya kutisha kidogo. Lakini wakati huo huo, kwa namna ya ajabu, nimejihisi salama na kulindwa. Studio yangu imekuwa kama bustani yangu. Tulishauriwa kwenda chini ya ardhi usiku wa kwanza kelele zilipoanza na tulilala huku tukiwa na mashuka mazito. Tunatumia eneo hili kwa busara.”