Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rio: Gerrard jiandae kuichukua Liverpool

Muktasari:

  • Gwiji wa Anfield, Gerrard ameambiwa ajiandae kwa ajili ya kwenda kuwa kocha wa muda wa Liverpool endapo kama Slot atashindwa kurekebisha mambo katika kikosi hicho.

LONDON, ENGLAND: RIO Ferdinand amemwambia staa mwenzake wa zamani wa England, Steven Gerrard kwamba ajiandae kwa ajili ya kupokea simu kutoka kwa mabosi wa Liverpool kwenda kuokoa jahazi kutokana na presha inayomkabili kocha Arne Slot kwa sasa.

Gwiji wa Anfield, Gerrard ameambiwa ajiandae kwa ajili ya kwenda kuwa kocha wa muda wa Liverpool endapo kama Slot atashindwa kurekebisha mambo katika kikosi hicho.

Licha ya kwamba Liverpool iliichapa West Ham United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England Jumapili iliyopita, vichapo vitatu mfululizo kwa mabao matatu, huku timu hiyo ikikabiliwa na ratiba ngumu hilo linamfanya Rio aamini kuna hatari ya Slot kupoteza ajira yake.

Rio Ferdinand alisema: “Nilikuwa nimekaa hapa na kumwambia Gerrard, 'ndugu unahitaji kuandaa vifaa vyako na jiweke tayari kwa ajili ya kwenda kuwa kocha wa mpito.' Hicho ndicho ninachofikiri. Kuna mechi nyingi sana zinakuja, sioni kama Slot atapenya kwenye mechi hizo zote kwa hali hii.”

Liverpool ilitarajia kumenyana na Sunderland kwenye mchezo wa Ligi Kuu England usiku wa jana Jumatano. Mabao mawili yaliyofungwa na Cody Gakpo na Alexander Isak kwenye mchezo dhidi ya West Ham yalirudisha ari kiasi kwenye kikosi hicho cha kocha Slot.

Lakini, kocha Slot amepoteza mechi tisa kati ya 13 zilizopita na hapo kuna mechi ya Inter Milan inakuja, kisha itapambana na Brighton na baadaye Tottenham kabla ya Krismasi.

Gerrard amekuwa hana kazi tangu alipofutwa kazi Al-Ettifaq, Januari. Aliiongoza timu hiyo ya Saudi Arabia kwa siku 55 tu.