Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rice awaza ubingwa Kombe la Dunia

RICE Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa kati anaamini timu ya taifa ya England ina vipaji vya kutosha ndani ya uwanjani na wamekuwa chini ya kocha mahiri, Thomas Tuchel, ambaye atakwenda kuwasaidia kubeba taji la Kombe la Dunia katika fainali zitakazofanyika Marekani mwakani.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO ghali wa Arsenal, Declan Rice amesema tena kwa msisitizo kwamba England haipaswi kuwa waoga wa kusema itakwenda kushinda taji la Kombe la Dunia.

Kiungo huyo wa kati anaamini timu ya taifa ya England ina vipaji vya kutosha ndani ya uwanjani na wamekuwa chini ya kocha mahiri, Thomas Tuchel, ambaye atakwenda kuwasaidia kubeba taji la Kombe la Dunia katika fainali zitakazofanyika Marekani mwakani.

Rice alikuwa sehemu ya kikosi cha England kilichocheza fainali mbili za Euro na sasa anaamini mastaa wa timu hiyo wana njaa ya kufikia mafanikio ya kubeba taji hilo kubwa.

England imekuwa timu ya kwanza ya Ulaya kukamatia tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2026 na imewekwa orodha ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kunyakua taji hilo.

Rice amesema: “Tunataka kushinda taji. Itakwenda kuwa ngumu. Lakini, sisi ni England. Tuna wachezaji wenye viwango katika kila eneo uwanjani.

“Kama hatuwezi kufikiria hilo, tutakuwa tumeweka akili ya udhaifu. Nadhani sota tunataka kushinda Kombe la Dunia. Nadhani Kombe la Dunia lililopita tulicheza vizuri sana, tulipoteza kwa Ufaransa, hakikuwa kitu kibaya.”

Rice alidai kwamba England ina utajiri wa vipaji kama Harry Kane na Jude Bellingham ambao wanacheza soka la viwango vya juu huko Bayern Munich na Real Madrid mtawalia, ambao wanawapa jeuri ya kwenda kuwa na timu ya ushindani kwenye fainali hizo za ubingwa wa dunia.