Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mfahamu Pina, nyota aliyeandika rekodi mpya Cape Verde

Muktasari:

  • Licha ya kikosi hicho kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Uruguay katika mechi ya kundi H, lakini bao la kwanza la Pina alilofunga kwa Frii-Kiki ya dakika 21, limemfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Cape Verde kufunga katika historia ya Kombe la Dunia inayoshiriki mwaka huu wa 2026 kwa mara ya kwanza.

FLORIDA, MAREKANI: KIUNGO wa Cape Verde, Kevin Lenini Gonçalves Pereira de Pina ameandika rekodi mpya baada ya Kuifungia timu hiyo bao la kwanza la historia ya kikosi hicho katika Fainali za Kombe la Dunia.

Licha ya kikosi hicho kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Uruguay katika mechi ya kundi H, lakini bao la kwanza la Pina alilofunga kwa Frii-Kiki ya dakika 21, limemfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Cape Verde kufunga katika historia ya Kombe la Dunia inayoshiriki mwaka huu wa 2026 kwa mara ya kwanza.

Katika mechi hiyo, Pina alifunga bao la kwanza la Cape Verde dakika 21, kwa Frii-Kiki kali, lingine likifungwa na Helio Varela huku yale ya Uruguay yakifungwa na Maximiliano Araujo na Agustín Canobbio.

Mchezaji huyo amezaliwa Januari 27, 1997, huko Praia, Cape Verde ambapo safari yake ya soka ilianzia nyumbani kwao akiwa mdogo kwenye akademi za ndani kama Tchadense kabla ya kwenda Ulaya ili kujaribu bahati yake.

Baada ya kucheza soka Cape Verde, Pina alihamia Ureno ambapo alijiunga na klabu ndogo ya Oliveirense ambayo baadaye ilimtoa kwa mkopo kwenda timu za Anadia na Sertanense ili iwe chachu ya kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara na kuonyesha kipaji chake.

Mwaka 2019, Pina alijiunga na Klabu ya GD Chaves ya Ureno ambapo nyota yake ilizidi kung'ara baada ya kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara tofauti na ilivyokuwa timu za mwanzo.

Kiwango bora alichokionyesha kikawa ni sehemu ya mafanikio yake baada ya mwaka 2022, maskauti wa  FC Krasnodar ya Urusi kuvutiwa na kipaji chake na kumsajili anakoendelea pia kucheza hadi sasa kwa kiwango bora.

Mwaka 2022, Pina alianza kuichezea timu ya taifa ya Cape Verde ambayo leo ameifungia bao la kwanza na la kihistoria katika Fainali za Kombe la Dunia zinazofanyika Marekani, Mexico na Canada, ambapo kikosi hicho maarufu kwa jina la 'Tubaroes Azuis' au 'Blue Sharks' (Papa wa Bluu) kinashiriki kwa mara ya kwanza mwaka huu 2026.