Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Refa wa Arsenal apewa gemu ya Barca Ulaya

Muktasari:

  • Mwamuzi, Oliver 39, amechaguliwa kuchezesha mechi ya Barcelona na Atalanta kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kesho Jumatano na anatarajia kurejea mzigoni kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu England wikiendi hii.

LONDON, ENGLAND: MWAMUZI, Michael Oliver ataonekana tena uwanjani kucheza mechi ya soka licha ya kuripotiwa kutumiwa meseji za vitisho kutokana na tukio lake la kumtoa kwa kadi nyekundu nyota wa Arsenal, Myles Lewis-Skelly.

Mwamuzi, Oliver 39, amechaguliwa kuchezesha mechi ya Barcelona na Atalanta kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kesho Jumatano na anatarajia kurejea mzigoni kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu England wikiendi hii.

Familia ya mwamuzi Oliver iliandamwa kwa meseji za vitisho kiasi cha kuwafanya polisi kuanza kuchunguza suala hilo jambo lililomfanya bosi wa zamani wa PGMOL, Keith Hackett kupendekeza mwamuzi huyo angepumzishwa kidogo.

Oliver aliwaambia mabosi wa Uefa na PGMOL anataka kuendelea na kazi yake ya kuchezesha kitu ambacho ameungwa mkono.

PGMOL ilitarajia kutangaza majina ya waamuzi kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu England jana Jumanne.

Oliver alifanya mazungumzo na bosi wa sasa wa PGMOL, Howard Webb juzi Jumatatu na kupewa sapoti zote. Ishu yake ya kuhusu vitisho imekabishwa kwa kitengo maalumu cha polisi wa soka Uingereza (UKFPU) kufanya uchunguzi wao.

Bosi wa UKFPU, Mark Roberts alisema: “Kama watu wanadhani wanaweza kujificha kwenye vicharazio vyao (keyboard) watakuwa wanajidanganya. Na tutawatafuta hata ng’ambo ya nchi kwa msaada wa maofisa wa nje.”

Oliver aliandamwa na meseji za vitisho vya maisha baada ya kumtoa kwa kadi nyekundu Lewis-Skelly kipindi cha kwanza katika mechi ambayo Arsenal iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wolves kwenye mchakamchaka wa Ligi Kuu England, Jumamosi iliyopita.