Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Refa aliyetimuliwa EPL, ageuka usafirishaji mizigo

Muktasari:

  • Coote mwenye umri wa miaka 42, alifukuzwa na Chama cha Waamuzi England (PGMOL), Desemba, mwaka jana baada ya kuonekana kwenye picha jongefu zilizovuja, ikiwemo moja ambapo alimkashifu kocha wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp na nyingine aliyoonekana akivuta unga mweupe.

LONDON, ENGLAND: MWAMUZI wa zamani wa Ligi ya England, David Coote ameonekana akifanya kazi ya kusafirisha mizigo ikiwa ni miezi kadhaa tangu aondolewe katika orodha ya waamuzi.

Coote mwenye umri wa miaka 42, alifukuzwa na Chama cha Waamuzi England (PGMOL), Desemba, mwaka jana baada ya kuonekana kwenye picha jongefu zilizovuja, ikiwemo moja ambapo alimkashifu kocha wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp na nyingine aliyoonekana akivuta unga mweupe.

PGMOL iligundua vitendo vya Coote vilifanya nafasi yake kama mwamuzi wa isiendelee na chama hicho kinachoongozwa na Howard Webb kilikatisha ajira yake mara moja.

Haikushia hapo, Coote pia alipigwa marufuku ya miezi 16 na UEFA Februari, mwaka huu, kwa kukiuka ‘kanuni za msingi za mwenendo mwema’ na kuharibu heshima ya mchezo wa soka na Ulaya kwa ujumla.

Coote hajaonekana mara nyingi hadharani tangu wakati huo, lakini taarifa ya The Sun ya Jumatatu ilionyesha mwamuzi huyo wa zamani akifanya kazi mpya iliyoibua hisia tofauti kwa mashabiki.

Katika video kupitia kengele ya mlango ya wanandoa nyumbani kwao, Coote alionekana akiwasilisha kifurushi kupitia kampuni ya usafirishaji mizigo midogo ya  Evri. Inaripotiwa kuwa Coote ameanza kufanya kazi kwenye kampuni ya usafirishaji karibu na nyumbani kwake huko Newark, Nottinghamshire na alipohojiwa kuhusu kazi yake hiyo mpya alisema: “Najitahidi tu kutafuta riziki halali, nataka kuendelea na maisha yangu.Najaribu kusonga mbele...”