Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Real Madrid yabadilisha gia angani kwa Trent

TETESI Pict

Muktasari:

  • Trent mwenye umri wa miaka 26, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika Juni 30 wakati michuano ya Kombe la Dunia inaanza Juni 14.

REAL Madrid wako tayari kuilipa Liverpool fidia ili kumchukua beki wa kulia wa timu hiyo na England, Trent Alexander-Arnold mara baada ya msimu huu kumalizika ili kumuingiza katika timu mapema na kujiandaa na michuano ya Kombe la Dunia kwa upande wa klabu.

Trent mwenye umri wa miaka 26, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika Juni 30 wakati michuano ya Kombe la Dunia inaanza Juni 14.

Awali, fundi huyu alidaiwa kuwa huenda angetua Madrid kwa usajili huru lakini sasa hilo litashindikana kwa sababu Madrid itamhitaji mapema.

Hakuna taarifa kamili juu ya kiasi gani cha pesa Liverpool itahitaji kama ada ya uhamisho ingawa inaweza kuwa chini ya Pauni 20 milioni ambayo matajiri hao wa Jiji la Madrid waliwasilisha Januari ili kumpata.


Benjamin Sesko

ARSENAL ndio inaongoza katika vita yake dhidi ya Tottenham ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia, Benjamin Sesko, mwenye umri wa miaka 21, katika dirisha lijalo.

Sesko ambaye msimu huu amecheza mechi 34 za michuano yote na kufunga mabao 17, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2029. Arsenal imekuwa ikicheza mechi zake za siku za hivi karibuni bila ya straika asilia baada ya nyota wao kuumia.


Viktor Gyokeres

MSHAMBULIAJI wa Sporting Lisbon na Sweden, Viktor Gyokeres, 26, ameonyesha hamu ya kutaka kuondoka Sporting mwisho wa msimu huu kwa ajili ya kujiunga na timu kubwa zaidi itakayomwezesha kutimiza ndoto zake kubwa kwa siku za usoni.

Gyokeres ambaye alitajwa sana kuwa huenda akatua Manchester United au Arsenal kutokana na kiwango anachoendelea kukionyesha akiwa na Lisbon, mkataba wake unamalizika mwaka 2028.


Alexander Isak

LIVERPOOL na Arsenal wana pesa za kutosha ambazo zitawawezesha kumudu kutoa ada ya uhamisho inayohitajika na Newcastle United ili kumuuza straika wao raia wa Sweden, Alexander Isak, mwenye umri wa miaka 25.

Kwa mujibu wa ripoti, Newcastle inahitaji kiasi cha pesa kisichopungua Pauni 150 milioni ili kumuuza Isak, ambaye amekuwa katika kiwango cha juu klabuni hapo.


Kobbie Mainoo

KIUNGO wa Manchester United, Kobbie Mainoo, 19,  amepanga kukataa ofa mpya ya mkataba kutoka Manchester United na badala yake anataka  kujiunga na timu ya nje ya England.

Man United ipo tayari kumuuza kinda huyu kwa kiasi cha pesa kisichopungua Pauni 70 milioni.

Mainoo anataka kukataa ofa ya mkataba mpya kwa sababu ni ndogo chini ya mabosi wanaobana bajeti OT.


Casemiro

MANCHESTER United wamepanga kumuuza kiungo wao raia wa Brazil, Casemiro, 33, katika dirisha lijalo ambapo mkataba wake utakuwa umebakisha mwezi mmoja kabla ya kumalizika.

Vigogo wa mashetani wekundu walikuwa wakihitaji kumuuza staa huyu anayewindwa na timu za Saudi Arabia Januari lakini mpango wao huo ulifeli.


Jonathan David

MSHAMBULIAJI wa Lille na Canada, Jonathan David, 25, anatamani zaidi kutua England katika dirisha lijalo mara baada ya mkataba wake kumalizika. David amekuwa katika rada za timu mbalimbali za England ikiwa pamoja na Manchester United, Tottenham, Chelsea na Newcastle.


Ederson

JUVENTUS inataka kusajili wachezaji watatu katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambao wote ni kutoka  Atalanta ambao ni pamoja na kiungo Ederson, mwenye umri wa miaka 25, washambuliaji, Ademola Lookman, 27, na Mateo Retegui, 25. Mabosi wa Juventus wanataka kusajili mastaa hawa ili kuboresha kikosi chao hususani kwenye ushambuliaji.