Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Caicedo awatoa jasho Chelsea

Muktasari:

  • Kiungo huyo amekuwa muhimu kwelikweli kwenye mipango ya kocha Enzo Maresca katika fainali hizo, ambapo sasa The Blues imetinga fainali baada ya ushindi wa mabao 2-0.

NEW JERSEY, MAREKANI: BENCHI la ufundi la Chelsea limebaki kwenye presha kubwa ya wasiwasi wa hali ya kiungo wake Moises Caicedo ambaye aliumia kwenye mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia la Klabu dhidi ya Fluminense usiku wa Jumanne.

Kiungo huyo amekuwa muhimu kwelikweli kwenye mipango ya kocha Enzo Maresca katika fainali hizo, ambapo sasa The Blues imetinga fainali baada ya ushindi wa mabao 2-0.

Kocha Maresca sasa anakuna kichwa juu ya utimamu wa kiungo wake huyo kabla ya fainali ya Jumapili, ambapo itawakutanisha dhidi ya mshindi wa mechi ya usiku wa Jumatano baina ya Paris Saint-Germain na Real Madrid.

Caicedo aliteguka kifundo cha mguu wakati alipokuwa akigombea mpira. Alipatiwa matibabu, lakini hakuweza kuendelea na mechi na sasa ameibua wasiwasi mkubwa kama atakuwa fiti kwenye fainali.

Maresca aliulizwa kama kiungo huyo atakuwepo, lakini ameshindwa kutoa jibu linaloeleweka, aliposema: “Nilimwambia Caicedo afanye kila analoweza ili awepo uwanjani Jumapili. Ngoja tuone.”

Hata hivyo, Chelsea ina machaguo ya kutosha kwenye eneo la kiungo baada ya kuwapo wachezaji Andrey Santos na Kiernan Dewsbury-Hall, ambao wote walitokea benchini dhidi ya Fluminense.

Staa mpya Joao Pedro alikuwa shujaa wa Chelsea alipofunga mabao mawili ikiwa ni mechi yake ya kwanza kuanza katika kikosi hicho cha Stamford Bridge.