Rasmi Ole afukuzwa United

Sunday November 21 2021
ole

MANCHESTER, ENGLAND. KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amefungashiwa virago baada ya kupokea kichapo cha cha kushtukiza dhidi ya Watford.
Man United ilipokea kichapo cha mabao 4-1 uwanja wa Vicarage dhidi ya kikosi cha Claudio Ranieri huku Harry Maguire akitolewa kwa kadi nyekundu.
Kipigo hicho ni cha tano Man United inakipata Ligi Kuu England chini ya Solskjaer msimu huu.
Darren Fletcher atakuwa kocha wa muda hadi mbadala wa Solskjaer atakapotikana.
Fletcher ataiongoza Man United akisaidiana na Michael Carrick kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi Villarreal, kabla ya kumenyana na Chelsea wikiendi ijayo.
Zinadine Zidane anapewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya Solskjaer endapo kama atakubali kuchukua mikoba yake.

Advertisement