Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford akomalia kusepa Man United

Muktasari:

  • Kwa kuwa Aston Villa haina nia ya kumpa dili la kudumu, mshambuliaji huyo na wawakilishi wake tayari wameanza mazungumzo ya makubaliano ya kudumu na Barcelona, ingawa haijajulikana kama klabu hiyo ya Hispania itakubali ada ya uhamisho iliyopunguzwa ya Pauni 29.8 milioni.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England na Manchester United, Marcus Rashford anadaiwa kuungana na wakala wake, Pini Zahavi kutia presha katika mpango wake wa kuondoka Old Trafford ikielezwa kwamba amemtaka aharakishe kumalizana na waajiri wake.

Kwa kuwa Aston Villa haina nia ya kumpa dili la kudumu, mshambuliaji huyo na wawakilishi wake tayari wameanza mazungumzo ya makubaliano ya kudumu na Barcelona, ingawa haijajulikana kama klabu hiyo ya Hispania itakubali ada ya uhamisho iliyopunguzwa ya Pauni 29.8 milioni.

Rashford, 27, hayupo katika mipango ya kocha wa Man United, Reuben Amorim, lakini taarifa za karibuni zinadai huenda akasitisha mpango wake wa kuachana naye kwa kuwa ameonyesha ubora tangu alipotua Aston Villa kwa mkopo. Mkataba wake unamalizika 2028.


Dean Huijsen

ARSENAL, Chelsea na Liverpool zinatajwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kuvunja kipengele cha Pauni 50 milioni kilichowekwa na Bournemouth kwa ajili ya beki wa kati, Dean Huijsen, 20. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania amekuwa ameiwezesha timu hiyo kukamatia nafasi ya nane kwenye msimamo wa EPL. Msimu huu amecheza mechi 30 za mashindano yote na mkataba wake unamalizika Juni 30, 2030.


Mohammed Kudus

KIUNGO wa West Ham United na Ghana, Mohammed Kudus, 24, ametua katika anga la Arsenal inayojiandaa kutoa ofa kubwa ya Pauni 59.7 milioni mwishoni mwa msimu huu ili kuinasa saini yake. Tangu alipotua West Ham United msimu uliopita akitokea Ajax, mchezaji huyo amekuwa tegemeo katika kikosi cha kwanza, ingawa mwenyewe anapenda zaidi kutua Liverpool. Mkataba wake unamalizika Juni 30, 2028.


Cristhian Mosquera

BEKI wa Valencia na Hispania, Cristhian Mosquera, 20, anayeuzwa Pauni 21.3 milioni ameingia katika anga za Chelsea inayomfukizia kwa ajili ya msimu ujao baada ya eneo la ulinzi kuanza kuyumba. Hata hivyo, wababe hao wa Darajani wanakumbana na upinzani kutoka Barcelona na Real Madrid. Mkataba wake unamalizika Jun 30, 2026.


Rayan Ait-Nouri

BEKI wa kushoto wa Wolverhampton Wanderers na Algeria, Rayan Ait-Nouri, 23, ni chaguo la kwanza la Manchester City dirisha lijalo la kiangazi baada ya kuonyesha kiwango bora msimu huu. Ait-Nouri alikuwa chaguo la kwanza la Tottenham Hotspur katika dirisha lililopita la usajili, ambapo mkataba wake unaomalizika Juni 30, 2026 ili kuuvunja timu inayomtaka italazimika kutoa zaidi ya Pauni 40 milioni.


Jorrel Hato

BEKI wa kimataifa wa Ajax na Uholanzi, Jorrel Hato ameingia kwenye orodha ya wachezaji wanaofukuziwa na Real Madrid msimu ujao akilengwa kwenda kushika mikoba eneo la kushoto. Hata hivyo, bahati mbaya kwa vigogo hao wa Hispania ni kwamba Arsenal, Chelsea na Liverpool nazo zinavutiwa na beki huyo mwenye umri wa miaka 19. Mkataba wake unaisha Juni 30, 2028.


Kevin de Bruyne

ASTON Villa bado ina mpango wa kumsajili kiungo wa Manchester City, Kevin de Bruyne, 33, ambaye ataondoka mwisho wa msimu huu. De Bruyne ambaye anahusishwa na baadhi ya timu za Marekani na Saudi Arabia anadaiwa kuwa bado ana mpango wa kuendelea kucheza soka la kiushindani. Mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.


Dusan Vlahovic

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Serbia na Juventus, Dusan Vlahovic yupo mbioni kuondoka mwisho wa msimu na ndiye chaguo la kwanza upande wa washambuliaji kwa Arsenal iliyoweka mezani Pauni 51.1 milioni. Vlahovic, 25, anayemaliza mkataba 2026, amekuwa akiwindwa na timu za England tangu dirisha lililopita.