Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Raphinha afunguka kuhusu Xavi

Muktasari:

  • Mbrazili huyo alisajiliwa na Barcelona ilipokuwa chini ya Xavi, lakini alijikuta akiwekwa benchi mara nyingi.

BARCELONA, HISPANIA: STAA wa Kibrazili, Raphinha amesema hakuwahi kuaminiwa na Kocha Xavi wakati alipokuwa akiinoa Barcelona - jambo lililomfanya apate shida sana Nou Camp.

Mbrazili huyo alisajiliwa na Barcelona ilipokuwa chini ya Xavi, lakini alijikuta akiwekwa benchi mara nyingi.

Raphinha alikuwa na kiwango bora sana alipokuwa Leeds United, jambo lililowafanya Barcelona kutumia Pauni 55 milioni kunasa huduma yake.

Lakini, baada ya kutua Nou Camp alijikuta akiingia na kutoka kwenye kikosi cha kwanza na hivyo kumfanya ashindwe kuwa na kiwango kizuri. Anadai alikuwa akianzishwa na kucheza mechi nzima kama tu hakukuwa na machaguo mengine, lakini kinyume cha hapo, Xavi alikuwa akinyanyua wachezaji wengine ili tu amtoe Raphinha.

Na joto zaidi liliibuka kwenye mechi dhidi ya Manchester United kwenye Europa League, wakati Mbrazili huyo alidhani alikuwa kwenye kiwango bora kabisa cha soka lake. Hata hivyo, alitolewa jambo lililomfanya Raphinha kuwa na hasira kwenye benchi kabla ya kufanya mazungumzo ya kuwekana sawa na kocha wake, ambayo hayakusaidia chochote.

Raphinha alisema: “Nilihisi si yeye wala wasaidizi wake waliokuwa wakiniamini. Hakuna hata mmoja. Nilikuwa tayari kucheza dakika 90 na nilifanya kila kitu, lakini nikijitahidi sana ilikuwa naishia dakika ya 60.”

Kwa sasa, Raphinha amekuwa mchezaji muhimu kwelikweli kwenye kikosi cha Barcelona huku akiwekwa kwenye orodha wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu.