Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PSG, Liverpool, Barcelona na Atletico kwenye vita ya nusu fainali UEFA

Muktasari:

  • Madrid iliikaribisha Bayern huku Arsenal ikiifuata Sporting na mshindi wa jana ataungana na washindi wa leo na Paris Saint-Germain (PSG) itamenyana na Liverpool, huku ndugu wawili kutoka Hispania, Barcelona na Atletico Madrid wakiwa na mechi ya kisasi.

PARIS/BARCELONA: BAADA ya jana Jumanne kushuhudia kipute cha Ligi ya Mabingwa Ulaya kikipigwa, leo Jumatano mtoko ni ulke ule na miamba ya soka inaonyeshana kazi kusaka tiketi ya nusu fainali.

Madrid iliikaribisha Bayern huku Arsenal ikiifuata Sporting na mshindi wa jana ataungana na washindi wa leo na Paris Saint-Germain (PSG) itamenyana na Liverpool, huku ndugu wawili kutoka Hispania, Barcelona na Atletico Madrid wakiwa na mechi ya kisasi.

PSG itaikaribisha Liverpool kwenye Uwanja wa Parc des Princes, Paris, ikikumbuka kichapo cha bao 1-0 nyumbani, msimu uliopita hatua ya 16 bora, kabla ya kwenda kupindua matokeo kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 4-1 na kusonga mbele.

Msimu huu, Liverpool imekuwa na matokeo mabovu hasa Ligi Kuu England na ilitolea robo fainali ya Kombe la FA na Manchester City kwa mabao 4-0 na kuzidi kuwaweka kwenye presha vijana hao wa Arne Slot kwa kuonekana dhaifu watakapokabiliana na vijana wa Luis Enrique.

Liverpool imepoteza mechi 15 katika mashindano yote msimu huu, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi tangu 2014-15 na imeshinda mechi moja katika mechi tano za mwisho katika mashindano yote.

Kwa upande mwingine, PSG iko kwenye kiwango bora zaidi na itaikaribisha Liverpool ikiwa imetoka kuichapa Toulouse mabao 3-1 kwenye Ligi Kuu ya Ufaransa huku nyota wao, Ousmane Dembele akifunga mara mbili kwenye mchezo huo.

PSG inatamba na rekodi nzuri dhidi ya vigogo wa England kwa miaka ya karibuni, ikitoka Chelsea jumla ya mabao 8-2 katika hatua ya 16 ya michuano hiyo, huku changamoto kubwa kwao ni kusonga mbele kwani kwa misimu mitano mfululizo kumeshuhudiwa bingwa mtetezi akiishia hatua ya robo fainali.

PSG haijapoteza katika mechi saba za mwisho za mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (imeshinda 6, sare 1), ikiwa ni moja ya rekodi ya juu kwa klabu za Ligi Kuu ya Ufaransa.

Katika mchezo huu, PSG itakosa huduma ya winga, Bradley Barcola huku Liverpool ikimkosa Alisson kutokana na majeraha huku akitarajiwa kurejea mshambuliaji wao, Alexander Isak.

Barcelona itaikaribisha Atletico Madrid Camp Nou kwenye mikiki mikiki hii baada ya kutoka kuichapa mabao 2-1 ugenini katika Ligi Kuu Hispania na ni moja ya mechi ya kuvutia Madrid ikitaka kwenda kulipa kisasi.

Barcelona ina historia ya kupoteza katika hatua kama hii katika michuano ya Ulaya dhidi ya Atletico Madrid na ilichapwa mabao  2-1 msimu wa 2013-14 na 3-2 msimu wa 2015-16.

Hata hivyo, Barcelona imeshinda mechi tano kati ya sita za hivi karibuni dhidi ya Atletico Madrid katika mashindano yote, ikiwa ni pamoja na ushindi wa mabao 2-1 Jumamosi iliyopita.

Barcelona kwa sasa ipo kwenye kiwango bora, haijapoteza katika mashindano yote kwa takribani miezi miwili sasa huku nyota wao, Lamine Yamal akiendelea kuonyesha kiwango cha juu. Timu hii yenye uwezo mkubwa wa ushambuliaji inaweza kuwa tishio kubwa kwa Atletico Madrid msimu huu.

Atletico Madrid, kwa upande wao, hawajashinda katika mechi tatu mfululizo, ikiwa ni pamoja na kipigo cha mabao 2-1 kutoka Barcelona. Timu ya Diego Simeone ipo nafasi ya nne kwenye La Liga huku nguvu zao kwa sasa wakizielekeza zaidi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na fainali ya Copa del Rey dhidi ya Real Sociedad.

Katika mchezo wa leo, Barcelona inaweza kukosa huduma ya Raphinha na Frenkie de Jong ambao wapo majeruhi huku Ronald Araujo akiwa na shaka kufuatia kushindwa kumaliza mchezo uliopita wa ligi huku kwa Atletico akitarajiwa kukosekana Jan Oblak.