Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PSG, Arsenal UEFA ni kimbembe

Muktasari:

  • Licha ya kucheza mechi kibao bila ya kupoteza kwenye Ligue 1 baada ya mechi 30, malengo ya PSG yapo kwenye kuisukuma nje Arsenal katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal.

PARIS, UFARANSA: Paris Saint-Germain imeweka matumaini yote ya kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, lakini mbele yao kimesimama kigingi kinachoitwa Arsenal.

Licha ya kucheza mechi kibao bila ya kupoteza kwenye Ligue 1 baada ya mechi 30, malengo ya PSG yapo kwenye kuisukuma nje Arsenal katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal.

Bao la mapema la Ousmane Dembele kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Jumanne iliyopita uwanjani Emirates, unaipa PSG faida ya kusonga mbele wakati itakapomenyana na kikosi hicho kinachonolewa na Mikel Arteta katika kipute cha Parc des Princes.

PSG na Arsenal kila moja inahitaji kufika fainali ya pili kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. PSG ilifika fainali msimu wa 2019-20, wakati Arsenal ilifanya hivyo 2005-06. Kihistoria iliposhinda mechi ya kwanza ya nusu fainali ugenini ni mara moja tu, PSG ilitolewa. Na kwa upande mwingine, Arsenal haijawahi kusonga mbele baada ya kupoteza mechi ya kwanza ya nusu fainali nyumbani.

PSG imeshinda mechi tatu kati ya nne za mwisho za Ligi ya Mabingwa Ulaya ilizocheza nyumbani, ikifunga mabao 14 katika ushindi huo. Lakini, ilikumbana na vipigo viwili Parc des Princes msimu huu dhidi ya Liverpool na Atletico Madrid.

Arsenal nayo ina matumaini makubwa baada ya kushinda mechi zao nne za mwisho ilizocheza ugenini kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

PSG inashika nafasi ya pili kwenye klabu za kutoka ligi tano kubwa za Ulaya kwa kufunga mabao 135 kwenye michuano yote, nyuma ya Barcelona iliyofunga mabao 160 msimu huu kabla ya kipute cha usiku wa jana Jumanne dhidi ya Inter Milan.

Miamba hiyo ya Ufaransa imepiga mashuti 1,012 ikiizidi Real Madrid iliyofanya majaribio hayo mara 970. Arsenal mafanikio yao ya karibuni kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ni kuisukuma nje Real Madrid na imekuwa na safu ngumu ya mabeki. Kwenye orodha ya timu zilizobaki kwenye Ligi Kuu England msimu huu, Arsenal ndiyo timu ngumu kufungika, lakini itakuwa kwenye mtihani mzito wa kukutana na fowadi ya PSG ambayo imekuwa moto kwa kutikisa nyavu.

Vikosi vinavyotarajiwa;

PSG: Donnarumma; Hakimi, Marquinhos, Pacho, Mendes; Ruiz, Vitinha, Neves; Doue, Ramos, Kvaratskhelia

Arsenal: Raya; Timber, Saliba, Kiwior, Lewis-Skelly; Odegaard, Partey, Rice; Saka, Merino, Martinelli