Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Postecoglou afunguka kufukuzwa

BIG Pict

Muktasari:

  • Postecoglu mwenye umri wa miaka 60, amekuwa na wakati mgumu tangu achukue mikoba ya Nuno Espirito Santos aliyefukuzwa mwanzoni mwa msimu huu.

NOTTINGHAM, ENGLAND: KOCHA wa Nottingham Forest, Ange Postecoglou amesema mashabiki wana haki kuzoea na kutaka afukuzwe sababu ndio wenye timu.

Postecoglu mwenye umri wa miaka 60, amekuwa na wakati mgumu tangu achukue mikoba ya Nuno Espirito Santos aliyefukuzwa mwanzoni mwa msimu huu.

BI 02

Hadi sasa kocha huyo ameiongoza Nottingham katika mechi sita na hajashinda hata moja ikitoka sare mara mbili na kupoteza nne.

Mashabiki walionyesha kuchoshwa na kiwango cha timu baada ya kupoteza mechi ya Europa League dhidi ya Midtjylland kwa mabao 3-2. Katika Ligi Kuu England timu hiyo inashika nafasi ya 17 ikiwa na pointi tano na inaweza kujikuta katika nafasi za kushuka daraja ikiwa itapoteza mechi ijayo dhidi ya Newcastle United.

BI 01

“Nimesikia. Wao ni mashabiki na wana haki ya kutoa maoni. Hakuna cha kushangaza katika soka tena. Lazima tuendelee mbele. Hatuwezi kuendelea kufikiria mechi hii. Lazima tuchukue hatua. Tuna mechi ijayo dhidi ya Newcastle, lazima tujiandae.”

Postecoglou amekuwa kocha wa kwanza Nottingham Forest katika miaka 100 kutoshinda mechi yoyote kati ya sita za mwanzo (sare 2, vipigo 4), tangu John Baynes alivyoshindwa kushinda mechi saba za kwanza Agosti-Septemba 1925. Kocha huyo raia wa Australia alisaini mkataba wa miaka miwili Septemba 9, mwaka huu na ikiwa Nottingham itaamua kumfukuza huenda akapata zaidi ya Pauni 6 milioni kama fidia ya kuvunjiwa mkataba.