Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi wajigeuza 'maskoti' msako dawa za kulevya Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Video iliyochapishwa kwenye akaunti rasmi ya TikTok ya Polisi wa Peru inaonyesha maofisa hao waliovalia vinyago kama 'maskoti' mwenye kipara anayewakilisha Marekani, na Maple, moose anayewakilisha Canada wakivunja geti kwa kutumia kifaa maalumu cha kuvunjia milango kabla ya kumkamata mwanaume aliyekuwa amevalia fulana nyeupe.

LIMA, PERU: POLISI wa Peru wametumia mbinu isiyo ya kawaida katika mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya, kwa kufanya operesheni maalumu mjini Lima wakiwa wamevalia mavazi ya vinyago rasmi vya Kombe la Dunia 2026.

Video iliyochapishwa kwenye akaunti rasmi ya TikTok ya Polisi wa Peru inaonyesha maofisa hao waliovalia vinyago kama 'maskoti' mwenye kipara anayewakilisha Marekani, na Maple, moose anayewakilisha Canada wakivunja geti kwa kutumia kifaa maalumu cha kuvunjia milango kabla ya kumkamata mwanaume aliyekuwa amevalia fulana nyeupe.

Video hiyo pia inaonyesha maofisa hao wakikamata pakiti za unga mweupe unaoshukiwa kuwa dawa za kulevya pamoja na bunduki, huku kukiwa na maelezo yanayosema: "Hali ya Kombe la Dunia: Operesheni yamalizika kwa kuanguka 'Pichichi'."

Kwa mujibu wa Polisi ngazi ya taifa, operesheni hiyo ilipangwa baada ya uchunguzi wa kina wa kiintelijensia kugundua chimbo hatari kwa dawa za kulevya, lakini ilikuwa ngumu kuingia bila kutambuliwa.

Polisi walimnasa mtuhumiwa aliyekuwa shabiki mkubwa wa soka na alikuwa akifuatilia kwa karibu matukio yote yanayohusiana na Kombe la Dunia wakati wa kukamatwa kwake.

Kanali Carlos Fredy Alcantara Obregon, mkuu wa Kikosi cha Green Squad, aliliambia shirika la habari la Associated Press: "Kutokana na kazi ya kiintelijensia iliyofanywa na timu yetu, tuliweza kubaini kwamba mtu tuliyekuwa tunakaribia kumkamata alikuwa shabiki sugu wa soka ambaye aliishi na kupumua kwa hamasa ya Kombe la Dunia."

"Kwa hiyo tuliwavalisha maofisa wa Green Squad mavazi ya maskoti wa Kombe la Dunia ili waweze kumkaribia bila kuibua shaka na kufanikisha ukamataji wake." Hata hivyo, Peru haishiriki fainali Kombe la Dunia baada ya kumaliza katika nafasi ya tisa kati ya timu 10 kwenye hatua ya kufuzu Amerika Kusini.