Pogba ahamia kwenye muvi

Muktasari:

  • Staa huyo wa Ufaransa alikumbana na adhabu hiyo, Februari baada ya kupimwa na kukutwa anatumia dawa zinazopigwa marufuku michezo, alipopimwa kwenye mechi ya Juventus, Agosti mwaka jana.

TURIN, ITALIA: Kiungo wa zamani wa Manchester United, Paul Pogba ameripotiwa kuhamia kwenye maigizo wakati huu akiwa anatumikia adhabu ya kufungiwa miaka minne kwenye soka.

Staa huyo wa Ufaransa alikumbana na adhabu hiyo, Februari baada ya kupimwa na kukutwa anatumia dawa zinazopigwa marufuku michezo, alipopimwa kwenye mechi ya Juventus, Agosti mwaka jana.

Pogba alikata rufaa kwenye makahama ya rufani ya michezo, akisisitiza hakutumia dawa hizo.

Hata hivyo, wakati akisuburi rufani yake, ripoti zinafichua Pogba atahamia kwenye dunia ya maigizo.

Kinachoelezwa ni Pogba anapiga picha za video za filamu inayokwenda na jina la 4 Zeros.

Filamu hiyo ni mwendelezo wa 3 Zéros, ambayo ilitoka mwaka 2002 na kinachoelezwa ni kwamba filamu hiyo atakayoshiriki Pogba, itatokea April mwakani.

Katika filamu hiyo, Pogba atacheza kama kocha kijana wa mchezo wa soka. Pogba kama atafeli kwenye rufani basi atakuwa nje ya uwanja hadi 2027.

Pogba alirejea Juventus mwaka 2022 kwa uhamisho wa bure baada ya kuachana na Manchester United kwa mara ya pili. Supastaa huyo alikuwamo kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoshinda ubingwa wa dunia 2018.