Pochettino awatuliza mashabiki

Friday September 17 2021
psg pic

PARIS, UFARANSA. MAURICIO Pochettino ameshangazwa na mashabiki walitoa povu, wakiwalaumu Kylian Mbappe, Lionel Messi na Neymar, kuwa chanzo cha kuambulia sare dhidi ya Club Brugge Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Paris Saint-Germain ililazimishwa sare ya bao 1-1 licha kuwepo nyota hao wakali eneo la hatari.
Pochettino alikiri mastaa hao walijitahidi kuikomboa PSG hawakupasa kulaumiwa kabisa.
“Wanahitaji muda kuzoena, bado hawajaelewena itachukua muda kidogo, sikufurahishwa na matokeo hayo, tunafahamu tunatakiwa kuongeza juhudi,”
Neymar, Messi na Mbappe wana thamani ya Pauni 361 milioni wakijumuishwa pamoja, lakini walishindwa kuonyesha cheche usiku wa kuamkia jana.

Advertisement