Pepe mwingine awindwa Arsenal

LONDON, ENGLAND. ARSENAL imeripotiwa kuwa na nia ya kumsajili winga mwingine wa Kibrazil, Eduardo Gabriel maarufu Pepe anayekipiga FC Porto.
Kwasasa Arsenal ina mpango wa kumuuza Nicolas Pepe, aliyejiunga tangu mwaka 2019 kwa kitita cha Pauni 72 milioni akitokea Lille ya Ufaransa.
Pepe ameshindwa kung’ara tangu alipotua klabuni hapo, huku Arsenal ikionyesha nia ya kumuuza kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Sevilla imekuwa ikihusishwa na Pepe lakini Arsenal ipo tayari kupata hasara kubwa endapo itaamuuza licha ya kumsajili kwa pesa ndefu.
Wakati Arsenal ikijiandaa kumuuza Pepe washika bunduki hao wa jiji la London, wanajiandaa kutuma ofa FC Porto kwaajili ya Mbrazil huyo.
Wakati huohuo Arsenal imeambiwa Pepe huyo wa Porto atawagharimu Pauni 60 milioni.