Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Partey ashinda kesi ya kubaka

Muktasari:

  • Partey alikuwa akikabiliwa na mashtaka dhidi ya wanawake wawili tofauti na shtaka moja la kumfanyia unyanyasaji mwanamke mwingine wa  tatu. Staa huyo wa kimataifa wa Ghana aliripotiwa kufanya matukio hayo kati ya 2021 na 2022 akiwa akiichezea Arsenal.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Thomas Partey hana hatia katika mashtaka yaliyokuwa yakimkabili ya kubaka na kufanya unyanyasaji.

Partey alikuwa akikabiliwa na mashtaka dhidi ya wanawake wawili tofauti na shtaka moja la kumfanyia unyanyasaji mwanamke mwingine wa  tatu. Staa huyo wa kimataifa wa Ghana aliripotiwa kufanya matukio hayo kati ya 2021 na 2022 akiwa akiichezea Arsenal.

Partey, 32, aliondoka Arsenal mwishoni mwa msimu uliopita baada ya mkataba wake kufikia tamati na kwenda kujiunga na Villarreal kwa uhamisho wa bure.

Aliingizwa kwenye dakika ya 78 kwenye mechi ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Tottenham katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumanne na alienda mahakamani Southwark Crown Court asubuhi iliyofuatia.

Partey aliingia mahakamani akiwa na suti nyeusi. Alitaja jina lake na umri kabla ya kusafishwa na kuambiwa hana hatia katika mashtaka yote sita.

Partey alifunguliwa mashtaka Julai, mwaka huu, siku nne tu baada ya mkataba wake Arsenal kufika tamati mwishoni mwa Juni. Polisi kwanza walipokea taarifa ya kuhusu tuhuma za kubaka, Februari 2022. Partey alitokea kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Westminster, Agosti 5, ambako alipewa dhamana ya masharti akidaiwa kufanya makosa kwa wanawake watatu na kwamba alitakiwa kutoa taarifa polisi kama anasafiri nje ya England na kuhakikisha anatoa taarifa za makazi yake muda wote.

Partey alijiunga na Arsenal akitokea Atletico Madrid 2020 kwa  Pauni 45 milioni na aliitumikia mara 167 na kufunga mabao tisa. Kwa sasa anaitumikia Villarreal, ambapo hadi sasa ameshaichezea mechi tano baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi.