Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Osimhen: Sisi Nigeria tuko tayari kwa vita

OSIMHEN Pict

Muktasari:

  • Mabingwa mara tatu wa AFCON sasa wamepangwa kukutana na Msumbiji katika hatua ya 16 bora na Osimhen ameonyesha imani kubwa sana kwa wachezaji wenzake.

RABAT, MOROCCO: MSHAMBULIAJI wa Nigeria na Galatasaray, Victor Osimhen, amesema kikosi cha Super Eagles kiko tayari kabisa kuikabili Msumbiji katika hatua inayofuata ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amecheza mechi zote tatu za Nigeria nchini Morocco na aliwaongoza wenzake kama nahodha katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Uganda katika mechi ya mwisho kukamilisha hatua ya makundi.

Mabingwa mara tatu wa AFCON sasa wamepangwa kukutana na Msumbiji katika hatua ya 16 bora na Osimhen ameonyesha imani kubwa sana kwa wachezaji wenzake.

Osimhen amesema Super Eagles ni kati ya timu kubwa zaidi barani Afrika, na timu nyingine zinapaswa kuwa na hofu zinapopangwa kucheza dhidi ya Nigeria.

Aliyekuwa mshambuliaji wa Napoli anafahamu kuwa Nigeria ni kati ya vinara wa kutwaa taji la AFCON, hasa baada ya kumaliza katika nafasi ya pili nchini Ivory Coast miaka miwili iliyopita.

“Ndiyo, ninaiona nchi yangu kama moja ya timu zinazopigiwa hesabu. Sisi ni kati ya timu zinazoogopwa zaidi katika mashindano haya. Timu yoyote inaweza kuja kucheza nasi,” amesema Osimhen alipozungumza na ESPN.

“Kama ni timu nzuri, inaweza kuvuka, lakini kama si nzuri, tunaweza kuisambaratisha timu yoyote kwa sababu kikosi hiki kina ubora wa kuumiza timu yoyote kubwa au nzuri kwenye mashindano haya.

“Tunaheshimu kila timu iliyofuzu kwenda hatua inayofuata, na yeyote tutakayekutana naye, ataona roho ya mapambano ya Nigeria.

“Hatua ya 16 bora itakuwa ngumu zaidi kuliko makundi, hivyo vijana wako tayari kutoa kila kitu. Timu iko tayari kukutana na mpinzani yeyote.

“Tunaheshimu kila timu inayofuzu, lakini hatumuogopi mtu yeyote. Hii ina maana kubwa si kwangu tu, bali kwa timu nzima na kwa Nigeria.

“Imekuwa muda mrefu tangu kombe hili lirejee Nigeria, na kila mazoezi tunapitisha ujumbe wazi kwamba tumekuja kuchukua kombe.

“Nalitaka kombe hili kwa kiwango sawa na kila nchi nyingine iliyokuja kulishinda. Ndiyo maana sisi kama wachezaji tunashirikiana kuhakikisha tunatimiza lengo hili.”