Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Oscar ahofia maisha yake, astaafu soka

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa Brazil ambaye pia amepita klabu za China, alitangaza kustaafu soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 34 mwishoni mwa wiki iliyopita.

SAO PAOLO,  BRAZIL: INATOSHA. Ndiyo,, nyota wa zamani wa Chelsea Oscar dos Santos Emboaba Junior ‘Oscar’, ameamua kutundika daruga ili kunusuru maisha yake kutokana na maradhi yanayomsumbua.

Kiungo huyo wa Brazil ambaye pia amepita klabu za China, alitangaza kustaafu soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 34 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Oscar alifanya hivyo akiamini ni wakati sahihi wa kunusuru maisha yake kutokana na tishio la kifo lililomuweka kitandani kwa muda.

Mchezaji huyo hajacheza tangu Novemba baada ya kuzimia wakati wa mazoezi ya klabu yake ya Sao Paulo, timu yake ya kwanza na ya mwisho katika soka la kulipwa.

“Nilitaka kutoa zaidi kwa Sao Paulo, nilitaka kucheza zaidi. Nafikiri bado nilikuwa na uwezo wa kucheza kutokana na umri wangu, lakini kwa bahati mbaya hili limetokea. Sasa nastaafu na nitaendelea kuishabikia Sao Paulo, nitaendelea na maisha yangu kama shabiki,”  ilisomeka taarifa ya klabu hiyo ya Brazil ambayo alikuwa na mkataba nayo hadi 2027.

“Nafunga ukurasa wa kazi iliyonipeleka sehemu nyingi duniani. Nawashukuru wote kwa upendo hasa mashabiki wa Sao Paulo walioniunga mkono tangu niliporudi na katika kipindi hiki kigumu ninachopitia.”

Oscar anastaafu akiwa amecheza mechi 556 za kulipwa, akifunga mabao 136 na kutoa asisti 203 katika ngazi ya klabu. Alichezea Sao Paulo vipindi viwili, Internacional, Chelsea na Shanghai SIPG.

Pia aliichezea timu ya taifa ya Brazil mara 48 na kufunga mabao 12, na alikuwa sehemu ya kikosi cha Olimpiki cha nchi yake 2012 jijini London.

Novemba, mwaka jana, alizimia wakati wa mazoezi hali iliyomfanya ahofie maisha yake na alielezea kwa hisia  kile alichopitia:

“Sasa niko vizuri kuzungumzia hili. Kila nilipokuwa nalizungumzia nilikuwa naumia sana kihisia. Nilifanya vipimo, kisha nikazimia - moyo, presha ilikuwa inashuka, moyo ulikuwa unasimama. Kisha (madaktari) walinipa huduma ya dharura ya moyo kwa dakika kadhaa.

“Nakumbuka tu kuzimia. Watu wanasema unapokaribia kufa, unatoka nje ya mwili. Nilihisi kitu kama hicho. Upo kama kwenye ndoto nzuri. Ni haraka sana. Kisha nilimuona mwanangu akisema, ‘rudi baba’.”