Onana azidi kutesa makipa EPL

Pamoja na Manchester United kuwa miongoni mwa timu zilizoruhusu mabao mengi kwenye Ligi Kuu England, kipa wa  timu hiyo, Mcameroon Andre Onana anaongoza kwa 'Cleensheet' na kuwaacha mbali makipa wa timu zilizoko kwenye nafasi sita za  juu.

Jana Jumapili, Onana aliisaidia timu yake ikiwa ugenini kutoruhusu bao akiwa golini kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Everton.

Man United katika mechi 13 ilizocheza hadi sasa ni timu pekee ambayo haijatoka sare, imepoteza mechi tano na kushinda nane ikiruhusu kufungwa mabao 16 sawa na yale iliyofunga.
Onana hajarususu bao katika mechi tano ambazo ni dhidi ya Everton jana, Luton, Fulham, Burnley na Wolves na zote ikishinda bao 1-0.

Onana anaungana na kipa Sam Johnstone wa Crystal Palace na Nick Pope (Newcastle), wote hawajaruhusu mabao katika mechi 13 msimu huu.