Ole ndio basi tena United

Pointi zakomba mkwanja wa makocha England

MANCHESTER, ENGLAND. KLABU ya Manchester United imefanya maamuzi ya kuachana na Ole Gunnar Solskjaer baada ya timu hiyo kupokea kichapo cha kushtukiza cha mabao 4-1, kwenye mechi ya Ligi Kuu England.
Baada ya kipigo hicho cha kushtua bodi ya Man United iliitisha kikao wa dharura kujadili hatima ya Solskjaer.
Kikao hicho kilidumu kwa muda wa masaa matano kwa bodi hiyo kukifikia makubaliano ya Solskjaer kutimuliwa kazi haraka iwezekanavyo.
Wakati huo huo wamiliki wa klabu huyo familia ya Glazer imeridhia kocha huyo kufukuzwa baada ya kikao cha bodi.
Man United imefungwa mechi saba katika mechi 13 walizocheza msimu huu, rekodi mbovu chini ya kocha huyo raia wa Norway.