Odoi agoma kuuzwa Chelsea

Tuesday July 20 2021
odoi pic

LICHA ya mabosi wa Chelsea kuhusishwa kuwa  wanataka kumtumia winga wao kutoka  England, Callum Hudson-Odoi, 20, kama sehemu ya mabadilishano ya kuipata saini ya winga wa Bayern Munich na Ufaransa,  Kingsley Coman, 25, katika dirisha lijalo, taarifa zimefichua kwamba jamaa anataka kuendelea kusalia kwenye kikosi na kupigania nafasi yake.
 Mkataba wa Odoi unamalizika mwaka 2024. Odoi haonekani kuwa kwenye mipango ya
Thomas Tuchel kwa msimu ujao.
Msimu uliopita alicheza mechi 37 za michuano yote na kufunga mabao matano, lakini kati ya hizo kwenye Ligi Kuu alicheza 23 pekee idadi ambayo ni ndogo.
Tuchel amekuwa bize kujenga  kikosi chake kwa msimu ujao ambapo anahitaji pia kuipata saini ya staa wa Borrussia Dortmund na kuna ripoti zilikuwa zinaeleza kwamba Odoi anaweza kutumika kama sehemu ya ofa.

Advertisement