Nyota Spain aandika rekodi mbovu Kombe la Dunia
Muktasari:
- Nyota huyo ameandika rekodi hiyo katika mechi ya kwanza ya ufunguzi ya kundi H la Kombe la Dunia kati ya Hispania dhidi ya Carpe Verde iliyopigwa kwenye Uwanja wa Atlanta, Marekani.
ATLANTA, MAREKANI: MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Hispania, Mikel Oyarzabal ameandika rekodi mpya ya kuwa mchezaji wa kwanza tangu mwaka 1966, kucheza dakika 30, za Kombe la Dunia la FIFA bila kugusa mpira hata mara moja.
Nyota huyo ameandika rekodi hiyo katika mechi ya kwanza ya ufunguzi ya kundi H la Kombe la Dunia kati ya Hispania dhidi ya Carpe Verde iliyopigwa kwenye Uwanja wa Atlanta, Marekani.
Mshambuliaji huyo anayecheza Klabu ya Real Sociedad ya Hispania, ameandika rekodi hiyo mbovu baada ya upinzani mkali kutoka kwa kikosi cha Cape Verde kutokana na kuonyesha soka safi la kujilinda.
Hispania imekutana na upinzani mkali kutoka kwa Cape Verde katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia iliyoisha kwa timu hizo kushindwa kutambiana na kutoka suluhu ya (0-0).
Suluhu hiyo ilitokana na juhudi za timu ya Carpe Verde iliyokuwa inacheza kwa mbinu ya kujilinda huku ikitengeza mashambulizi zaidi kwa njia ya kushtukiza, huku shujaa wa kikosi hicho akiwa ni kipa Josimar Jose Evora Dias 'Vozinha'.