Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Scotland ataka Wirtz apigwe bei

Muktasari:

  • Katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, Liverpool ilivunja rekodi yake ya usajili kwa kumsajili Wirtz kutoka Bayer Leverkusen kwa ada inayoripotiwa kufikia Pauni 116 milioni, usajili ulioibua matumaini makubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo, lakini hadi sasa kiungo huyo, 22 hajaonyesha kiwango kilichotarajiwa.

LIVERPOOL, ENGLAND: NYOTA wa zamani wa Scotland, Craig Burley, ameishauri Liverpool kufikiria kumuuza kiungo mshambuliaji Florian Wirtz kutokana mwanzo mgumu wa maisha yake katika Uwanja wa Anfield.

Katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, Liverpool ilivunja rekodi yake ya usajili kwa kumsajili Wirtz kutoka Bayer Leverkusen kwa ada inayoripotiwa kufikia Pauni 116 milioni, usajili ulioibua matumaini makubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo, lakini hadi sasa kiungo huyo, 22 hajaonyesha kiwango kilichotarajiwa.

Msimu wa 2025/26 umekuwa mgumu kwa Wirtz huku Liverpool ikipitia kipindi cha matokeo yasiyoridhisha chini ya kocha Arne Slot. Katika mechi 37 alizocheza kwenye mashindano yote, Wirtz amefunga mabao sita na kutoa pasi nane za mabao, takwimu ambazo baadhi ya wachambuzi wanaona hazilingani na kiwango chake wala thamani ya usajili wake.

Akizungumza kabla ya mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham Hotspur, Burley ambaye aliwahi kuchezea Chelsea na Celtic, alisema amechoshwa na mjadala kuhusu mchezaji huyo.

“Tuache kuzunguka kwenye suala la Florian Wirtz. Nimechoka. Alichofanya Ujerumani ni historia sasa. Katika timu hii ya Liverpool anaonekana mwepesi sana na anakosa uthubutu katika eneo la mwisho,” alisema.

Alihoji pia kutoweka kwa sifa zilizomfanya ang’ae akiwa Leverkusen, akisema: “Kama si mabao, basi pasi ziko wapi? Ziko wapi zile chenga zake za kuwapita wachezaji watatu au wanne na kufunga?”

Burley aliongeza Wirtz anaweza kucheza vizuri zaidi kama namba 10, lakini kama hatarudi kwenye kiwango chake, Liverpool italazimika kufikiria kumuuza.

Hata hivyo, Wirtz awali alisisitiza bado anaendelea kuzoea mazingira mapya. Akizungumza na BBC mapema mwaka huu, alisema alianza msimu akiwa na presha ya kufanikiwa haraka lakini sasa anajisikia vizuri zaidi.